Hoteli za Sheraton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hoteli ya Sheraton ya Dubai
Hoteli ya Sheraton ya Atlantic City
Hoteli ya Sheraton ya Cairo
Hoteli ya Sheraton ya Hanoi

Hoteli za Sheraton ndiyo rajamu kubwa kabisa na inachukua nafasi ya pili baada ya Westin katika ukongwe baina ya hoteli zote za Starwood. Makao makuu ya Starwood ni katika White Plains, New York.

Historia ya Sheraton[hariri | hariri chanzo]

Asili ya jina la rajamu hii ni mwaka wa 1937 ambapo Ernest Henderson na Robert Moore walinunua hoteli ya Stonehaven huko,Springfield,Massachusetts. Hoteli hizi zilipata jina lao kutoka hoteli moja ya kitambo ambayo hawa wawili walikuwa wamenunua.Hoteli hiyo ilikuwa na ubao uliomulikwa na taa ndogo na kuonyesha jina "Sheraton Hotel".Ubao huo ungekuwa ghali kung'oa kwa sababu ya uzito wake.Hivyo basi,wakaamua kuita hoteli zao zote kwa jina hilo.

Henderson na Moore walikuwa wamefungua hoteli tatu kule Boston ilipofika mwaka wa 1939, waliendelea na upanuzi wa haraka huku wakinunua vipande vya ardhi kando ya pwani nzima ya Mashariki huko Marekani. Mnamo mwaka wa 1945,hoteli za Sheraton ilikuwa ni hoteli ya kwanza kuwa katika soko la hisa la New York.

Hapo mwaka wa 1949,hoteli za Sheraton ilipanuka katika mipango ya kimataifa kwa ununuzi wa hoteli za Canada mbili. Katika mwaka wa 1960,hoteli za Sheraton ziliendelea kuongezeka huku wakifungua hoteli ya kwanza nje ya Amerika ya Kaskazini kwa ufunguzi wa Tel Aviv-Sheraton katika mwezi wa Februari 1961 na Macuto-Sheraton nje ya Caracas, Venezuela katika mwaka wa 1963. Ilipofika mwaka wa 1965,hoteli ya 100 ya Sheraton ilijengwa. Kundi la kimataifa la ITT ilinunua hoteli zote za Sheraton,hapo mwaka wa 1968,kisha hoteli hizo zilijulikana kama ITT Sheraton.

ITT Sheraton walifanikiwa sana katika mwaka wa 1985 ilipokuwawa kampuni ya kwanza ya nchi za Magharibi kuendesha hoteli katika Jamhuri ya Watu wa Uchina na kuchukua usimamizi wa hoteli ya serikali iliyoitwa Hoteli ya Great Wall mjini Beijing, ambayo ikawa Great Wall Sheraton.

Katika mwaka wa 1994, ITT Sheraton ilinunua hisa nyingi katika kampuni ya Kiitaliano CIGA(Compagnia Italiana Alberghi Grandi) ama Kampuni ya Italian Grand Hotels.Kampuni ya CIGA ilikuwa imekamatwa na wakopeshaji kutoka kwa mmiliki wake wa awali,Aga Khan, kwa ajili ya kutolipa madeni. Kampuni ya ITT Sheraton ilianza kufungua hoteli Uitaliani kwanza alafu ikaanza kuendesha hoteli nyingi zaidi katika bara la Uropa kabla ya uchumi wa ulimwengu uanze kufeli. Hizi hoteli zilianzisha msingi wa lile lilokuja kuwa Kundi la ITT Sheraton Luxury, baadaye likaitwa Starwood's Luxury Collection.

Mnamo mwezi Aprili 1995, Sheraton ilianzisha hoteli mpya ambazo si ndogo sana wala si kubwa ili ichukue nafasi za hoteli zilizojulikana kama Sheraton Inns.

Miaka tatu baadaye (1998), Starwood Hotels & Resorts Worldwide Inc. ilinunua Kampuni ya ITT Sheraton (ilishinda kampuni ya Hilton iliyotaka kuinunua pia). Tangu hapo imekuwa ikinawiri na kuwa mojawapo wa kampuni za hoteli zinazoongoza duniani kote. Majina mengine ndani ya kampuni hii ni Four Points ya Hoteli za Sheraton,Hoteli za St. Regis,Luxury Collection,Element ya Westin,Le Méridien na Hoteli za W na kampuni ya Aloft.

Tangu kununua hoteli za ITT Sheraton, Starwood imeunda jina jipya kutoka hoteli zao. Hoteli za St. Regis zimepewa jina lao kutoka hoteli maarufu iliyo katika Fifth Avenue mjini New York,ambayo imekuwa hoteli ya Sheraton kwa miaka. Hoteli hiyo na Sheraton ya zamani iliyokuwa Carlton,Washington D.C. ndizo zilizokuwa hoteli za kwanza katika Hoteli za Sheraton zilizotandaa kote ulimwenguni.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: