Hope & Faith
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Hope & Faith | |
|---|---|
![]() Nembo ya Hope & Faith |
|
| Aina | Mchezo wa kuchekesha |
| Imetungwa na | Joanna Johnson |
| Nchi inayotoka | Marekani |
| Lugha | Kiingereza |
| Ina misimu | 3 |
| Utayarishaji | |
| Muda | makisio ni dk. 30 |
| Urushaji wa matangazo | |
| Kituo | ABC |
| Inarushwa na | 26 Septemba, 2003 |
| Viungo vya nje | |
Hope & Faith ni kipindi cha kuchekesha cha Marekani iliyoonyeshwa kuanzia Septemba 26, 2003 hadi Mei 2, 2006 kwa misimu mitatu kwenye stesheni ya ABC.
Kipindi hiki kilikuwa na waigizaji wakuu: Faith Ford na Kelly Ripa. Hope Shanowski (Ford) alikuwa na mume na watoto watatu. Faith Fairfield (Ripa) alikuwa muigizaji maarufu na nduguye Hope. Kipindi hiki inatokana na maisha ya mbunifu Joanna Johnson - ambaye alikuwa mhusika katika kipindi maarufu cha The Bold and the Beautiful. Kipindi hiki kilishirikisha wasanii wengine kama Tony Curtis, Dean Cain, Robert Wagner, Regis Philbin, Kathie Lee Gifford, Jenny McCarthy, Jaclyn Smith, Louise McCafferty na Mark Consuelos.
Kipindi hiki kilirekodiwa mjini New York City kwenye Silvercup Studios.
Yaliyomo |
[hariri] Mafanikio yake
| Msimu | Vipindi | Ilianza | Ilimalizika | Watazamaji (in milioni) |
Namba | |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 2003-2004 | 25 | Septemba 23, 2003 | Mei 14, 2004 | 8.23[1] | |
| 2 | 2004-2005 | 26 | Septemba 24, 2004 | Mei 6, 2005 | 6.94[2] | |
| 3 | 2005-2006 | 22 | Septemba 30, 2005 | Mei 2, 2006 | 5.8[3] | |
[hariri] Wahusika Wakuu
- Hope Fairfield-Shanowski (Faith Ford). Hope ndiye mama wa familia. Ameolewa na Charley na ana watoto watatu: Sydney, Haley, na Justin. Anapenda kupika na kupanda miti kwenye bustani lake.
- Faith Fairfield (Kelly Ripa). Faith ni nduguye Hope. Yeye ni mvivu, na anamfanya Hope amtendekeze. Mara kwa mara, anazua vitimbi na kumshirikisha nduguye. Yeye amejaribu kutafuta kazi kama mwigizaji, lakini hakufaulu.
- Charley Shanowski (Ted McGinley). Charley ni mumewe Hope. Yeye hampendi Faith, na kila mara anajaribu kumfukuza Faith kwenye nyumba. Yeye ni daktari wa meno na anapenda kuangalia michezo.
- Sydney Shanowski (Nicole Paggi). Sydney ni mtoto wa kwanza wa Hope na Charley. Yeye anampenda Faith zaidi ya mamake.
- Hayley Shanowski (Macey Cruthird). Hayley ni mwana wa pili wa Hope na Charley. Ni mtoto mwerevu aliyerukishwa hadi darasa la kidato cha pili. Yeye ni mwenye huruma na anapenda wanyama.
- Justin Shanowski (Jansen Panettiere). Ni mwana wa mwisho. Ni mtoto mwerevu anayempenda babake na Faith sana.
[hariri] Marejeo
- ↑ Viewership numbers of primetime programs during the 2003-04 television season. Archived from the original on 2007-02-08. Retrieved on 2007-11-06.
- ↑ Season Program Rankings from 09/20/04 through 05/22/06. ABC Medianet (May 24, 2005). Rudishwa juu ya 2009-07-03.
- ↑ http://www.hollywoodreporter.com/hr/search/article_display.jsp?vnu_content_id=1002576393
[hariri] Viungo vya nje
- Hope & Faith katika Internet Movie Database
