Historia na Maendeleo ya Mji wa Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dar es Salaam ilikuwa ikiitwa “Mzizima”(Ikimaanisha mji wenye neema), ni mji wa zamani ulioanza mwanzoni mwa miaka ya 1857. Ingawa historia ya Mzizima ilianza tangu miaka 1000 iliyopita ambapo watu wa Barawa (ambao walijichanganya na Wazaramo na kuwa kati yao) ambao walitulia na kulima katika maeneo ya mbwa maji magogoni (kwa sasa kivukoni), Mjimwema na Gezaulole.

Jiji la Dar es Salaam

Mji ulianza kuonesha mabadiliko kutokana na ujio wa wa Masultani, Wajerumani na Waingereza. Mwaka 1866 Sultan Seyyed Majid of Zanzibar aliupa jina la ambalo ndilo linalotumika sasa neno la kiarabu lililomaanisha “Mbingu ya Amani”. Baaba ya kifo cha Sultan Majid mwaka 1870, Dar es Salaam ilianguka lakini iliinuka tena mara baada ya ulio wa kampuni ya Kijerumani (German East Africa Company) iliyoanzisha kituo cha biashara mwaka 1887 na kuuondoa utawala wa Kiarabu hata kutawala pwani ya Africa Mashariki.

Walijenga mamlaka kwa ajili ya kusimamia mambo malimbali ndani ya Africa Mashariki na kuanzisha biashara kwa ajili ya maendeleo ya njia ya reli ya kati.

Iliweza kukua kwa haraka kutokana na utawala pamoja na biashara ya Wajerumani Afrika ya Masahriki. Mwaka 1891 ulikuwa mji mkuu wa “Gerrnan East Africa“.

Dar es Salaam zamani Mzizima, ni mji mkubwa katika Tanzania na unapatikana pembezoni mwa bahari ya Hindi. Ni mji mashuhuri na ni muhimu kwani ni mji wa Kibiashara.

Jiji la Dar es Salaam

Wakati wa vita ya kwanza ya dunia Wajerumani Afrika Mashariki waliangushwa na Waingereza na tangu hapo ilijulikana kama Tanganyika. Baada ya vita vya pili vya dunia, Dar es Salaam ilikuwa kwa haraka ikiwepo kuanzishawa kwa chama cha TANU(Tanganyika African National Union) ambacho kilisababisha Tanganyika kujipatia uhuru tarehe 9 Desemba 1961.

Dar es Salaam iliendelea kuwa mji mkuu mpaka ulipohamishiwa Dodoma mwaka 1973 , ambao ni mji ulio katikati ya nchi ya Tanzania. Licha ya kutokuwa na tawala za mji mkuu lakini Dar es Salaam iliendelea kuwa makao makuu ya serikali.

Historia ya Ujerumani bado imekuwa ikionekana katika mji. Dar es Salaam ni mji muhimu kwa biashara na serikali.