Guinea (kanda)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
--Kwa maana mbalimbali za neno Guinea angalia Guinea (maana)--
Ramani ya Kiingereza ya Afrika ya Magharibi, mnamo mwaka 1736

Guinea ni jina la kihistoria kwa ajili ya kanda ya kusini ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa Sahara na Atlantiki. Nchi zote kuanzia Senegal hadi kaskazini ya Angola zilihesabiwa kuwa "Guinea". Waandishi wa Ulaya walitofautisha "Guinea ya Juu" (Senegal hadi Kamerun) na "Guinea ya Chini" (Kamerun hadi Angola).

Majina ya kihistoria kwa Afrika ya Magharibi[hariri | hariri chanzo]

Lugha za Ulaya zilikuwa na majina ya kihistoria kwa ajili ya sehemu mbalimbali za pwani la Guinea ya Juu: Pwani la Pilipili (ing. "Pepper Coast"), Pwani la Meno ya Ndovu (ing. Ivory Coast), Pwani la Dhahabu (ing. Gold Coast) na Pwani la Watumwa (ing. Slave Coast). Majina haya yametokana na biashara kuu katika sehemu zile. Jina la "Pwani la Meno ya Ndovu" linaendelea kutumika katika nchi ya Cote d'Ivoire (Ivory Coast). Ghana lilitwa "Gold Coast" (Pwani la Dhahabu) hadi uhuru.

Asili ya jina "Guinea"[hariri | hariri chanzo]

Jina la "Guinea" limetokana na jina la kale kwa ajili ya sehemu kubwa ya upande wa kusini ya Afrika ya Magharibi likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya kiberber. Maelezo mengine yasema ni umbo la jina "Ghana" kutokana na ufalme wa kale.

Historia ya pamoja[hariri | hariri chanzo]

Nchi za eneo hili zilishiriki katika biashara ya kimataifa kwa kuwasiliana na Afrika ya Kaskazini na dunia ya Kiislamu kwa biashara ya misafara ya Sahara lakini pia kwa kuwasiliana na Ulaya kupitia Atlantiki.

Biashara ya meno ya ndovu, dhahabu na watumwa ilitajirisha falme za pwani zilizopata nafasi ya kujenga enzi yao. Nchi hizi karibu na pwani zilikuwa ndogo kuliko falme kubwa za Sahel lakini zilikuwa na watu wengi na nguvu ya kisiasa pia kijeshi.

Vituo vya nchi za Ulaya kwa muda mrefu zilikuwa ndogo tu za kusaidia biashara kwanza ya watumwa baadaye ya mawese kwa mahitaji ya mapinduzi ya viwanda Ulaya. Mwisho wa karne ya 19 BK eneo lote liliingia katika kipindi cha ukoloni ya Kiulaya.

Jina la Guinea leo[hariri | hariri chanzo]

Jina la Guinea linatumika leo kwa ajili ya nchi tatu za Guinea, Guinea-Bisau na Guinea ya Ikweta barani Afrika. Linatokea tena katika kawaida ya lugha mbalimbali kama majina ya kijiografia ya kutaja "ghuba ya Guinea", "misitu ya Guinea", "nyanda za juu za Guinea" na kadhalika.

Kisiwa kikubwa cha Guinea Mpya karibu na Australia pamoja na nchi ya Papua Guinea Mpya ndani yake vimepokea jina kutokana na ile "Guinea ya awali" barani Afrika.

Nchi za Kanda la Guinea ya Juu[hariri | hariri chanzo]

Nchi za Kanda la Guinea ya Chini[hariri | hariri chanzo]

Mito[hariri | hariri chanzo]

Kati ya mito mikubwa ya kanda Guinea kuna Niger na Kongo.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]