Gran Canaria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Gran Canaria
Gran Canaria kutoka angani

Gran Canaria ni kisiwa cha Kihispania kwenye funguvisiwa la Visiwa vya Kanari katika bahari ya Atlantiki mbele ya mwambao wa Afrika ya Magharibi.

Mji mkuu pia mji mkubwa ni Las Palmas de Gran Canaria kaskazini mwa kisiwa.

Uchumi wa Gran Canaria kama wa funguvisiwa lote unategemea hasa utalii. Kusini mwa kisiwa kuna kitovu cha utalii kwenye sehemu za Maspalomas na Playa Inglis.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kina umbo la duara lenye kipenyo cha km 45  na eneo la km² 1,560. Idadi ya wakazi ni mnamo 800,000.

Gran Canaria ipo kati ya visiwa vya jirani vya Tenerife na Fuerteventura kwenye 28° 0' N na 15° 35' W. Mahali pa juu ni volkeno ya Pico de las Nieves yenye kimo cha mita 1,949 juu ya UB.

Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Gran Canaria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.