Goregore
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Goregore | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Goregore, gegemela au vinuka ni ndege wa jenasi Phoeniculus katika familia Phoeniculidae. Hawa ni ndege weusi wenye mkia mrefu na domo refu jekundu au jeusi lililopindika. Mwangani kwa jua manyoya yao yana mng'ao kijani au zambarau wa metali. Kuna mabaka meupe kwa mabawa na mkia. Hupenda kuwa kwa makundi na hupiga kelele pamoja mara kwa mara wakitetea. Inaelekea kama sauti yao ni asili ya jina “gegemela”. Hula wadudu ambao wanawatafuta katika nyufa za miti kama vigong'ota. Jike huyataga mayai 2-4 ndani ya tundu asilia ya mti au tundu ya zuwakulu au kigong'ota. Baina ya kundi la kama ndege kumi ipo jozi moja tu inayozaa. Ndege wengine wasaidia hawa wawili kutunza makinda.
Spishi za Afrika [hariri]
- Phoeniculus bollei, Goregore Kichwa-cheupe (White-headed Wood Hoopoe)
- Phoeniculus castaneiceps, Goregore-misitu (Forest Wood Hoopoe)
- Phoeniculus damarensis, Goregore Zambarau (Violet Wood Hoopoe)
- Phoeniculus granti, Goregore wa Grant (Grant's Wood Hoopoe)
- Phoeniculus somaliensis, Goregore Domo-jeusi (Black-billed Wood Hoopoe)
- Phoeniculus purpureus, Goregore Kijani (Green Wood Hoopoe)