Go-Tsuchimikado
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Go-Tsuchimikado (3 Julai, 1442 – 21 Oktoba, 1500) alikuwa mfalme mkuu wa 103 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Fusahito. Tarehe 21 Agosti, 1464 alimfuata baba yake, Go-Hanazono, na kuwa mfalme hadi kifo chake. Aliyemfuata ni mwana wake, Go-Kashiwabara.

