Gertrudi wa Thuringia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Gertrudi wa monasteri ya Helfta (1256 – 17 Novemba 1301) alikuwa mtawa wa kike nchini Ujerumani.
Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu kama bikira. Sikukuu yake ni 16 Novemba.
[hariri] Maisha
Gertrudi alizaliwa katika mji wa Eisleben, mkoa wa Thuringia, nchini Ujerumani mwaka 1256.
Katika utoto wake alilelewa na watawa wa kike Wabenedikto wa urekebisho wa Citeaux huko Helfta, ambako alifaulu vizuri katika masomo yake, hasa falsafa, historia na fasihi.
Alijiweka kabisa mikononi mwa Mungu, akasonga mbele haraka sana katika utakatifu, akitumia muda wake katika kusali na kufanya fikara.
Alikufa tarehe 17 Novemba, mwaka 1301.
[hariri] Tazama pia
[hariri] Marejeo
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1570
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gertrudi wa Thuringia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |