Gerimani
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Gerimani |
|
|---|---|
| Jina la Elementi | Gerimani |
| Alama | Ge |
| Namba atomia | 32 |
| Mfululizo safu | Simetali |
| Uzani atomia | 72.64 |
| Valensi | 2 na 4 |
| Kiwango cha kuyeyuka | 1211.40 K (938.25 °C) |
| Kiwango cha kuchemka | 3106 K (2833 °C) |
| Asilimia za ganda la dunia | 6 · 10-4 % |
| Hali maada | mango |
Gerimani (kutoka kilat. "Germania" kwa nchi ya Ujerumani alikotoka mfumbuzi wa elementi hii) ni nusumetali au metaloidi yenye namba atomia 32 katika mfumo radidia. Uzani atomia ni 72.64.
Tabia [hariri]
Gerimani ni dutu mango na ngumu yenye rangi nyeupe-fedha.
Matumizi [hariri]
Ilikuwa muhimu kama nusukipitishio katika transista hadi silikoni imetumiwa zaidi badala ya Gerimani.
Siku hizi hutumiwa sana katika teknolojia ya inforedi inaposaidia kutengezwa kwa darubini za usiku au kamera za inforedi.