Gaua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani za kisiwa cha Gaua
Gaua kati ya visiwa vya Vanuatu

Gaua ni kisiwa cha Vanuatu. Zamani kiliitwa Santa Maria. Kiko upande wa kusini wa kisiwa cha Vanua Lava. Eneo la kisiwa ni 342 km². Kijiji kikubwa kabisa kisiwani huitwa Jolap. Mwaka wa 2009 idadi ya watu kisiwani imehesabiwa kuwa 2491. Lugha za asili ambazo huzungumzwa kisiwani kwa Gaua ni Kilakon, Kiolrat, Kidorig, Kinume na Kikoro.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.