Gamalieli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Gamalieli alikuwa kiongozi wa kabila la Manase anayetajwa katika Biblia ya Kiebrania, ambayo ni sehemu ya Biblia ya Kikristo (Agano la Kale), katika kitabu cha Hesabu, sura ya 2, mstari wa 20.

Muhimu zaidi ni Gamalieli mwingine, Gamalieli I au Gamalieli mzee, kiongozi wa Mafarisayo katika karne ya 1 B.K. Anatajwa katika Agano Jipya, ambayo ni sehemu ya pili ya Biblia ya Kikristo, kama mwalimu wa mtume Paulo aliyewatetea mitume wa Yesu. Mapokeo ya Ukristo yanamheshimu kama mtakatifu). Katika Talmud ya Uyahudi anatajwa kwa heshima kama Rabban Gamliel.

Saint-stub-icon.jpg Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gamalieli kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.