Five Years Gone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Five Years Gone"
Sehemu ya Heroes

Hiro wa Baadaye anaelezea kuhusu mustakabalis.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 20
Imetungwa na Joe Pokaski
Imeongozwa na Paul Edwards
Tayarisho la 120
Tarehe halisi ya kurushwa 30 Aprili 2007
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
".07%" "The Hard Part"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Five Years Gone" ni sehemu ya ishirini ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa kipindi cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na televisheni ya NBC, Heroes. Hiki ni kipengele cha mwisho kabla ya vipande vitatu vya mwisho vya msimu wa kwanza. Sehemu hii awali ilijulikana kama "String Theory." Jina lilibadilishwa na kuwa "Five Years Gone", na "String Theory" ilitumika kama jina la Ukurasa wa 30 kwenye riwaya za picha za Heroes. [1]

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Sehemu hii inahusu hasa juu ya Hiro Nakamura na Ando Masahashi wakisafiri miaka mitano baadaye, inaonesha mahali dunia itakapokuwa iwapo mlipuko wa bomu hautozuiwa. Hiro wa Baadaye, mara iliyopita alivamia kwenye kipengele cha "Hiros", kipengele maarufu sana, wakati huu amekuwa kama gaidi mkubwa wa dunia na mkuu wa Battōjutsu. Ando aliuawa kwenye mlipuko, ambapo kwa mujibu wa Peter, hiyo ndiyo sababu Hiro amepoteza upande wake wa uchale na kuwa na uchungu wa kubadilisha yaliyopita.

Nathan Petrelli kwa sasa ni Rais wa Marekani, na Mohinder Suresh akiwa kama Mshauri Mkuu wa Masuala ya Afya na Matt Parkman akiwa kama Mkuu wa Usalama wa Taifa akiwa na Haitian ubavuni kwake. Niki Sanders amekuwa menenguaji tena, anajiita "Jessica", jina la alter ego wake wa zamani na dada'ke, ikiwa kama jina la kisanii. Mtoto wake Micah aliuawa kwenye mlipuko ambao umeharibu kwa kiasi kikubwa mji wa New York. Niki ana uhusiano wa kimapenzi na Peter Petrelli, ambaye ana kovu la shavu lisilioonekana vizuri katika upande wa shavu la kushoto.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. TV Recap: Heroes - Chapter 20 - Five Years Gone
  2. "String Theory". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-04-30. Iliwekwa mnamo 2007-03-26. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]