Firigogo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Firigogo | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Firigogo ni ndege wa nyika wa jenasi Pterocles na Syrrhaptes katika familia Pteroclididae. Wataalamu wengine wanawaainisha katika jenasi moja Pterocles. Wanafanana kidogo na njiwa lakini ni wanono kuliko hawa. Wana rangi za kamafleji, kwa sababu hukitafuta chakula kwa tambarare wazi. Manyoya ya tumbo, yale ya dume hasa, yamerekebishwa kufyonza maji. Hii inawezesha ndege kuwabebea makinda maji. Hula mbegu, zile za Leguminosae hasa na pia punje za nafaka. Jike huyataga mayai 2-4 chini ndani ya tundu ya kina kifupi.
Spishi ya Afrika [hariri]
- Pterocles alchata, Firigogo Mkia-pini (Pin-tailed Sandgrouse)
- Pterocles bicinctus, Firigogo Mikufu-miwili (Double-banded Sandgrouse)
- Pterocles burchelli, Firigogo wa Burchell (Burchell’s Sandgrouse)
- Pterocles coronatus, Firigogo Taji (Crowned Sandgrouse)
- Pterocles decoratus, Firigogo Uso-mweusi (Black-faced Sandgrouse)
- Pterocles exustus, Firigogo Tumbo-jekundu (Chestnut-bellied Sandgrouse)
- Pterocles gutturalis, Firigogo Koo-njano (Yellow-throated Sandgrouse)
- Pterocles lichtensteinii, Firigogo wa Lichtenstein (Lichtenstein’s Sandgrouse)
- Pterocles namaqua, Firigogo wa Namakwa (Namaqua Sandgrouse)
- Pterocles orientalis, Firigogo Tumbo-jeusi (Black-bellied Sandgrouse)
- Pterocles personatus, Firigogo wa Madagaska (Madagascar Sandgrouse)
- Pterocles quadricinctus, Firigogo Mikufu-minne (Four-banded Sandgrouse)
- Pterocles senegallus, Firigogo Madoadoa (Spotted Sandgrouse)
Spishi za mabara mengine [hariri]
- Pterocles indicus (Painted Sandgrouse)
- Syrrhaptes paradoxus (Pallas’s Sandgrouse)
- Syrrhaptes tibetanus (Tibetan Sandgrouse)