Kozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Falconidae)
Kozi
Kozi tembere
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Falconiformes (Ndege kama kozi)
Familia: Falconidae (Ndege walio na mnasaba na kozi)
Leach, 1820
Ngazi za chini

Nusufamilia 3, jenasi 11:

Kozi ni ndege mbuai wadogo wa familia ya Falconidae.

Wana mabawa membamba yaliyochongoka ambayo yanawapa uepesi na uwezo wa kubadilisha mwelekeo upesi. Kozi tembere, ndege wepesi kabisa duniani, wanaweza kufikia kasi ya kushuka ya zaidi ya km 300 kwa saa.

Kozi hula mawindo madogo kama ndege, panya, mijusi na wadudu. Spishi nyingine hutumika sana kwa uwindaji kwa ndege mbuai.

Jike hutaga mayai juu ya miamba, ndani ya mianya, juu ya tawi kubwa au ndani ya tago la ndege mwingine kama kunguru. Mara nyingi hawatumii vijiti au vitu vingine kujenga tago salihi.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]