Felix Eboue

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Félix Éboué)
Gavana Mkuu Eboué anamkaribisha Charles de Gaulle nchini Chad.
Mchoro wa Felix Eboué iliyochorwa na Charles Alston, 1943.

Félix Adolphe Éboué (26 Desemba 1884 - 17 Machi 1944) alikuwa Mfaransa Mweusi aliyezaliwa Guyani ya Kifaransa na alikuwa kiongozi wa kikoloni na pia wa Wafaransa Huru.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Cayenne, akiwa mjukuu wa watumwa na alikuwa mwana wa nne katika familia ya ndugu watano. Baba yake, Yves Urbain Eboué, alikuwa na kipawa cha kuongelesha watu na mama yake, Marie Josephine Aurélie Leveillé, alikuwa muuzaji kwa duka alikuwa amezaliwa Roura. Marie Josephine aliwalea watoto wake kwa mila za guiana creole. Eboué alikuwa mwanafuzi mwenye kipaji ambaye alishinda udhamini ya kusoma katika shule ya sekondari katika mji wa Bordeaux,Ufaransa. Eboué pia alikuwa mchezaji wa kandanda na alikuwa nahodha wa timu ya shule yake iliyosafiri kucheza katika michuano mle Ubelgiji na pia kufika Uingereza.

Baada ya kufuzu katika masomo ya kisheria kutoka École Coloniale,Paris, yeye alifanya kazi katika Oubangui-chari kwa miaka ishirini na kisha huko Martinique. Katika mwaka wa 1936 alifanywa kuwa kiongozi wa mkoa wa Guadeloupe, na akawa ntu mweusi wa kwanza kuteuliwa kwa cheo cha juu hivo popote katika makoloni ya Ufaransa.

Baada ya miaka miwili,migogoro ilipoanza kumtatiza, alihamishiwa kuenda Chad, aliwasili katika Fort Lamy tarehe 4 Januari 1939. Yeye alikuwa muhimu sana katika kuendeleza msaada wa Chad kwa Wafaransa Huru katika mwaka wa 1940, ni hatua ambayo hatimaye ilimpa kikundi cha Charles de Gaulle nguvu za kuendesha biashara zake kwa makoloni yote mengine ya Ufaransa katika sehemu za Afrika zilizokuwa karibu na ikweta. Akiwa gavana wa eneo hilo zima katika miaka ya 1940-1944, Eboué alitenda ili kuboresha hadhi ya Waafrika,kwa mfano aliwatenga Waafrika 200 waliosoma kama wenye thamanina kupunguza kodi zao.Vilevile,aliwaajiri watumishi waliotoka Gabon(waliofanya kazi katika sekta za kiraia) katika nyadhifa za mamlaka. Yeye pia alichukua hatua ya kujihusisha katika kazi ya watu ambao baadaye wangekuwa muhimu katika njia zao tofauti, mifano ni Jean-Hilaire Aubame na Jean Remy Ayouné.

Ingawa alikuwa Francophile aliyekuza lugha ya Kifaransa katika [Afrika],makala yake ya La nouvelle politique indigène("Sera Mpya ya Waafrika") aliyochapisha 8 Novemba 1941,alitetea utunzaji wa taasisi za jadi za Kiafrika.

Yeye alikufa kwa shtuko la moyo akiwa [Cairo]; makoloni ya Kifaransa yalitoa stempu ya makumbusho ya Felix Eboue. Afisa wa Jeshi la Heshima,aliyekuwa ametuzwa katika mwaka wa 1941 na Msalaba wa Ukombozi na alikuwa mwanachama wa Baraza la Amri ya Ukombozi,majivu yake Felix yako katika Panthéon,akiwa mtu mweusi wa kwanza kupewa hiyo heshima.

Mahali pa Félix-Éboué palipo 12th arrondissement ya Paris na pia Stesheni ya Metro ya Paris Daumesnil (Paris Métro) ni makumbusho ya kumpa heshima Félix Éboué. Yeye pia ana njia ndogo katika jina lake karibu na La Défense.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]