Euphrase Kezilahabi
Euphrase Kezilahabi (amezaliwa 13 Aprili 1944 katika kijiji cha Namagondo kisiwani Ukerewe) ni mwandishi kutoka nchi ya Tanzania. Lugha yake ya kwanza ni Kikerewe lakini huandika hasa kwa Kiswahili ambacho amekipanua kwa kutumia mitindo ya lugha yake ya asili.
Yaliyomo |
Maisha [hariri]
Euphrase Kezilahabi alizaliwa 13 Aprili 1944 huko Namagondo kisiwani Ukerewe kilichopo ndani ya Ziwa Viktoria. Babake Vincent Tilibuzya alikuwa msimamizi wa kijiji na Euphrase alikuwa na ndugu 10 yaani wavulana 5 na wasichana 5. Alisoma shule ya msingi ya Nakasayenge halafu tangu 1957 Seminari ya kikatoliki ya Nyegezi aliyomaliza mwaka 1966. [1]
1967 alijiandiskisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akasoma ualimu na fasihi hadi digrii ya B.A. katika mwaka 1970. Mwaka uleule 1970 akawa mwalimu wa shule ya sekondari Mzumbe (Morogoro) halafu kwenye shule ya sekondari ya Mkwawa (Iringa).
1971 alirudi chuoni Dar es Salaam akawa mhadhiri msaidizi wa chuo alipoandika pia tasinifu ya M.A. kuhusu riwaya za Shaaban Robert, tangu 1974 mhadhiri kamili na 1978 mhadhiri mwandamizi. Akaendelea na masomo ya Ph.D. huko Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison alipotoa tasinifu yake mwaka 1985 kuhusu "African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation". Sasa (mwaka 2012) ni profesa wa lugha za Kiafrika kwenye Chuo Kikuu cha Botswana.
Maandiko [hariri]
Baadhi ya maandiko yake ni:
Riwaya:
- Rosa Mistika (1971)
- Kichwamaji (1974)
- Dunia Uwanja wa Fujo (1975)
- Gamba la Nyoka (1979)
- Nagona (1987/1990)
- Mzingile (1991)
Mashairi:
- Kichomi (1974)
- Karibu Ndani (1988)
- Dhifa (hakijatolewa bado)
Tamthiliya:
- Kaptula la Marx (1978/1999)
Marejeo [hariri]
- ↑ Noronha analeta habari kuhusu maisha yake tangu utotoni hadi kuwa mhadhiri, mengine katika "profile" (taz. chini)
Viungo vya Nje [hariri]
- Euphrase Kezilahabi kwenye Britannica online
- Profile of Euphrase Kezilahabi
- [http://www.swahili-literatur.at/nacherzaehlungen/rosamistika.pdf Lourenco Noronha, Euphrase Kezilahabi 1971 Rosa Mistika (kwa lugha ya Kijerumani), Taasisi ya Taaluma ya Bara la Afrika, Chuo Kikuu cha Vienna, Mei 2009 (iliangaliwa Januari 2013)
- Blogu juu ya tamthiliya yake "Kaptula la Marx
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Euphrase Kezilahabi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |