Eta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Sho 90
Heta 8 Koppa 90
Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Eta ni herufi ya saba katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama η (alama ya kawaida) au Η (alama kubwa). Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu, ikiwa alama ya namba 8.

Asili ya Eta ni herufi ya Kifinisia ya kheta (tazama makala ya H). Matamshi yake ya awali yalikuwa "h" na kwa maana hiyo alama iliingia katika alfabeti ya Kietruski na ya Kilatini. Ndani ya Kigiriki chenyewe sauti ya "h" ilipotea kwa muda na alama ilibaki kama "eta" ikimaanisha sauti ya aina ya "e".

Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki, eta inatumiwa kama kifupisho kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fizikia.

Katika fizikia eta ni alama kwa mesoni ambayo ni kipande kidogo cha atomi.