Erwin Schrödinger
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Erwin Schrodinger)
Erwin Schrödinger (12 Agosti, 1887 – 4 Januari, 1961) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Austria. Hasa alichunguza sifa za mawimbi ndani ya nadharia ya kwanta. Mwaka wa 1933, pamoja na Paul Dirac alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

