Enzi ya kati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kanisa la Mt. Michael mjini Hildesheim (Ujerumani) ni mfano bora wa usanifu wa enzi ya kati

Enzi ya Kati (pia: Zama za Kati) ilikuwa kipindi cha historia ya Ulaya kati ya mwisho wa Dola la Roma mnamo mwaka 500 na matengenezo makuu ya kanisa mnamo mwaka 1500.

Historia ya Ulaya hugawanywa mara nyingi katika vipindi vitatu vya Enzi ya Kale, Enzi ya Kati na Enzi ya Kisasa. Hata kama ugawaji huu umetokana na mazingira ya Ulaya tu hutumiwa pia kwa maeneo mengine ya dunia. Wataalamu wengi huamini ya kwamba haufai sana kidunia lakini hadi sasa hakuna mpangilio mwingine kwa dunia yote unaoeleweka kirahisi hivi.

Mwanzo wa kipindi cha Enzi ya Kati[hariri]

Kabla ya Enzi ya Kati kulikuwa na ustaarabu wa Dola la Roma. Milki hii kubwa ilijenga utamaduni uliounganisha nchi za Afrika ya Kaskazini, Asia ya Magharibi na Ulaya ya Kusini pamoja na Ulaya ya Magharibi. Katika eneo hili kubwa palikuwa na uchumi ulioendela na njia za mawasiliano kama barabara, mabandari hata aina ya posta. Ustaarabu huu ulikuwa na idadi ya watu waliojua kusoma na kuandika. Lugha za pamoja kama Kilatini na Kigiriki zilieleweka na asilimia fulani ya watu kote katika dola hili. Hata kama watu wengi hasa watu wa vijijini na watumwa hawakujua kusoma bado walikuwepo watu waliojua kila sehemu ya dola.

Ustaarabu huu uliporomoka pamoja na matatizo ya kiuchumi, gharama kubwa kwa jeshi na mashambulio ya makabila ya nje hasa ya Wagermanik yaliyoweza kuingia ndani ya Dola la Roma bila kulingana na utamaduni wa ustaarabu huo. Roma ilishindwa kutunza utaratibu wake mbele ya mashambulio na uhamiaji huo.

(ya kuendelea)

Viungo vya Nje[hariri]

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Enzi ya kati kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.