Eneo Bunge la Tetu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo Bunge la Tetu ni eneo bunge la uchaguzi nchini Kenya. Ni mojawapo wa maeneo bunge sita katika Wilaya ya Nyeri, Mkoa wa Kati.
Eneo Bunge la Tetu linajumuisha Taarafa ya Tetu katika Wilaya ya Nyeri. Eneo Bunge la Tetu lote liko katika eneo la Baraza la Mji wa Nyeri. Eneo bunge hili lilianzishwa kwa ajili ya uchaguzi wa 1988.
Wangari Maathai amekuwa mbunge wa Tetu tangu uchaguzi wa 2002 . Alituzwa Tuzo la Amani la Nobel mwaka wa 2004.
Yaliyomo |
Wabunge[hariri]
| Mwaka wa Uchaguzi | Mbunge [1] | Chama | Vidokezo |
|---|---|---|---|
| 1988 | Nahashon Kanyi Waithaka | KANU | Mfumo wa Chama kimoja. |
| 1992 | Joseph Gethenji | Democratic Party (DP) | |
| 1997 | Paul Gikonyo Muya | Democratic Party (DP) | |
| 2002 | Wangari Maathai | NARC | |
| 2007 | Francis Nyammo | Party of National Unity (PNU) |
Wadi[hariri]
| ' | |
| Wadi | Wapiga kura waliosajiliwa |
|---|---|
| Aguthi | 14,571 |
| Karundu | 9,708 |
| Muhoya | 5,719 |
| Tetu | 6,494 |
| Thingingi | 7,756 |
| Jumla | 44,248 |
| *Septemba 2005 | [2],[3] | |
Marejeo[hariri]
- ↑ Center for Multiparty Democracy: Politics and Paliamenterians in Kenya 1944-2007
- ↑ Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency
- ↑ Electoral Commission of Kenya: Civic Elections Results (2002)