Eneo Bunge la Dagoretti
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo Bunge la Dagoretti ni eneo bunge le uchaguzi nchini Kenya. Ni mojawapo wa maeneo bunge nane katika Mkoa wa Nairobi. Linajumuisha vitongoji vya magharibi vya Nairobi. Eneo Bunge la Dagoretti lina mipaka sawia na Taarafa ya Dagoretti ya Nairobi. Eneo lote la bunge hili liko katika eneo la Baraza la Mji wa Nairibi. Lina ukubwa wa eneo wa kilomita mraba 39 . Lilikuwa linajulikana kama Eneo Bunge la Nairobi West katika uchaguzi wa mwaka wa 1963 ,lakini jina lake lilibadilisdhwa hadi la sasa kuanzia uchaguzi wa 1969.
Yaliyomo |
Wabunge [hariri]
| Mwaka wa Uchaguzi | Mbunge [1] | Chama | Vidokezo |
|---|---|---|---|
| 1963 | Njoroge Mungai | KANU | |
| 1969 | Njoroge Mungai | KANU | Mfumo wa Chama kimoja. |
| 1974 | Johnstone Muthiora | KANU | Mfumo wa Chama kimoja. Muthiora punde baada ya kuchaguliwa [2]. |
| 1975 | Francis Kahende | KANU | Uchaguzi mdogo, Mfumo wa Chama kimoja. |
| 1979 | Njoroge Mungai | KANU | Mfumo wa Chama kimoja. |
| 1983 | Clement Gachanja | KANU | Mfumo wa Chama kimoja. |
| 1988 | Chris Kamuyu | KANU | Mfumo wa Chama kimoja. |
| 1992 | Chris Kamuyu | FORD-Asili | |
| 1997 | Beth Wambui Mugo | Social Democratic Party | |
| 2002 | Beth Wambui Mugo | NARC | |
| 2007 | Beth Wambui Mugo | Party of National Unity (PNU) |
Kata na Wadi [hariri]
| Kata | |
| Kata | Idadi ya Watu* |
|---|---|
| Kawangware | 86,824 |
| Kenyatta/Golf course | 30,253 |
| Mutuini | 14,521 |
| Riruta | 65,958 |
| Uthiru/Ruthimitu | 23,016 |
| Waithaka | 19,937 |
| Jumla | 240,081 |
| Sensa ya 1999 [3]. | |
| Wadi | |
| Wadi | Wapiga kura waliosajiliwa |
|---|---|
| Kawangware | 22,662 |
| Kenyatta/Golf course | 24,948 |
| Mutuini | 6,344 |
| Riruta | 20,329 |
| Uthiru/Ruthimitu | 8,120 |
| Waithaka | 6,952 |
| Jumla | 89,355 |
| *Septemba 2005| [4]. | |
Marejeo [hariri]
- ↑ Center for Multiparty Democracy: Politics and Paliamenterians in Kenya 1944-2007
- ↑ Daily Nation, August14, 2003: Debate on PM is as old as Kenya
- ↑ information.go.ke: CDF allocation by sector and location (2003-6)
- ↑ Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency