Emil Theodor Kocher
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Emil Theodor Kocher (25 Agosti, 1841 – 27 Julai, 1917) alikuwa daktari mpasuaji kutoka nchi ya Uswisi. Alifanya na kuboresha pasuaji nyingi, hasa ya tezi dundumio. Mwaka wa 1909 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.

