Embu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Embu | |
| Mahali pa mji wa Embu katika Kenya | |
| Anwani ya kijiografia: 0°32′0″S 37°27′0″E / 0.53333°S 37.45°E | |
| Nchi | Kenya |
|---|---|
| Mkoa | Mashariki |
| Wilaya | Embu |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 41,092 |
Embu ni mji mdogo wa Kenya upande wa kusini-mashariki wa Mlima Kenya. Umbali na Nairobi ni 120 km. Embu ni makao makuu ya Mkoa wa Mashariki na pia ya wilaya ya Embu.
Kuna wakazi 41,100. Mji uko kwa kimo cha mita 1,350 juu ya UB. Uliundwa na walowezi Waingereza mnamo 1906.
Kuna asilimia kubwa ya watumishi wa serikali hapa wanaofanya kazi kwenye ofisi za mkoa pia katika shule nyingi zilizopo.