Elizabeth Ann Seton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Elizabeth Ann Seton

Elizabeth Ann Bayley Seton (28 Agosti, 17744 Januari, 1821) alikuwa mwanzilishi wa shirika la Masista wa Huruma wa Mt. Yosefu (kwa Kiingereza Sisters of Charity of St. Joseph), ambalo lilikuwa utawa wa kwanza kuundwa huko Marekani. Hasa alifundisha na kuwasaidia watoto maskini wengi.


[hariri] Maisha yake

Elizabeth Ann Bayley alizaliwa New York katika familia ya ushirika wa Anglikana: tarehe 25 Januari 1794, akiwa na umri wa miaka 19, aliolewa na mfanyabiashsara tajiri William Seton, akamzalia watoto watano.

Alipobaki mjane tarehe 27 Desemba 1802) alifunga safari ya kiroho iliyomfanya aongokee Kanisa Katoliki tarehe 25 Machi 1805.

Akahamia Baltimore, chini ya askofu John Carroll, akaanza utume wake kwa wanawake wajane wenye watoto wadogo na kuanzisha shule nyingi.

Tarehe 1 Juni 1809 alianzisha shirika la kitawa lenye kufuata roho ya Vinsenti wa Paulo akahamia Emmitsburg, kwenyeMaryland: mwaka 1812 alipokea katiba ya Mabinti wa Upendo wa Mt. Vinsenti wa Paulo, iliyorekebishwa na kuidhinishwa na askofu Carrol. Kundi ls kwanza la masista (mama Seton na wenzake 16) waliweka nadhiri zao za daima tarehe 19 Julai 1813.

Alifariki mwaka 1821.

[hariri] Heshima aliyopewa

Mchakato wa kumtangaza mwenyeheri ulianza mwaka 1907 na kumalizika Papa Yohane XXIII alipomtangaza tarehe 17 Machi 1963. Tarehe 14 Septemba 1975 Papa Paulo VI alimtangaza kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 4 Januari.


[hariri] Viungo vya nje

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine