Elisha
Elisha (kwa Kiebrania אֱלִישַׁע, Elisha, yaani "Mungu wangu ni wokovu", kwa Kigiriki Ἐλισσαῖος, Elissaios au Ἐλισαιέ, Elisaie, kwa Kiarabu الْيَسَع Elyasaʿ) alikuwa nabii anayetajwa katika Biblia na katika Qur'an.
Katika Biblia [hariri]
Elisha alifanya unabii wake katika ufalme wa kaskazini wa Israel wakati wa wafalme Yoram, Yehu, Yehoahaz na Yehoashi [1]
Elisha alikuwa mwana wa Shaphat kutoka Abel-meholah aliyepata kuwa mfuasi wa nabii Elia (Kitabu cha kwanza cha Wafalme 19:16–19).
Baada ya huyo kuchukuliwa mbinguni katika kisulisuli (Kitabu cha pili cha Wafalme 2:9), Elisha alikubaliwa kama mkuu wa wanafunzi wake ("wana wa manabii") akajulikana nchini kwa karama zake, zikiwa ni pamoja na uponyaji.
Kwa miaka karibu sitini (892 – 832 hivi KK) alikuwa nabii (2Fal 5:8), akijihusisha sana na siasa akaombwa shauri na wafalme mbalimbali hata wa nchi za nje. Kwa kumpaka mafuta Yehu alianzisha mapinduzi dhidi ya ukoo wa Ahabu na kukomesha upotoshaji wake wa imani. Mapinduzi hayo yakaenea kusini kwa kumuua Atalia, binti wa Yezebeli, aliyetawala miaka saba kisha kuua watu wote wa ukoo wa Daudi (mtoto Yoashi tu alinusurika).
Tanbihi [hariri]
- ↑ Achtemeijer, Paul L. ed., and Dennis R. Bratcher, Ph.D. "Elisha." HaperCollins' Bible Dictionary. New York, New York: HarperCollins Publishers, 1996.
Viungo vya nje [hariri]
- Elisha katika Internet Movie Database – Animated depiction of the life of Elisha
- "Eliseus" article from The Catholic Encyclopedia
- Prophet Elisha in Carmelite Tradition
- Prophet Elisha Orthodox icon and synaxarion