E pluribus unum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maneno ya E pluribus unum yaonekana kwenye kanda mdomoni mwa tai katika nembo la Marekani

E Pluribus Unum ni kaulimbiu ya Marekani inayopatikana kwenye nembo la taifa na kwenye noti ya dolar moja.

Kaulimbiu hiyo ni kutoka lugha ya Kilatini likimaanisha "Moja kutoka wengi" yaani Umoja umetokana na maungano ya pande mbalimbali. Neno limechaguliwa kwa sababu lilionyesha umoja wa makoloni 13 yaliyoasi Uingereza na kuwa chanzo cha Marekani.