Do You

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Do You”
“Do You” cover
Kasha ya wimbo wa Do You
Single ya Ne-Yo
kutoka katika albamu ya Because of You
Imetolewa 12 Juni 2007/24 Julai (USA), 2007
(Ufalme wa Muungano), 30 Julai 2007
(Ujapani), 21 Novemba 2007 (akimsh. Utada)
Muundo Radio Airplay/CD single, 12" single
Imerekodiwa 2007
Aina R&B, pop
Urefu 3:48
Studio Def Jam Recordings
Mtunzi Allen, M./Smith, S./Sparkman, M.
Mtayarishaji The Heavyweights
Single za Ne-Yo na tarehe zake
"Because of You"
(2006)
"Do You"
(2007)
"Can We Chill"
(2007)


Single za Utada na tarehe zake
"Beautiful World / Kiss & Cry"
(2007)
"Do You"
(2007)
"Heart Station / Stay Gold"
(2008)

"Do You" ni wimbo wa 2007 ulioimbwa na mwimbaji-mtunzi wa R&B Ne-Yo. Wimbo unamzungumzia Ne-Yo akiwa anajaribu kumwuliza mwanamke wake wa zamani kuwa keshawahi kumfikiria kabisa. Ni wimbo wa pili kutoka katika albamu yake ya pili ya Because of You.

Wimbo ulitolewa rasmi katika maredio kunako tarehe 12 Juni 2007. Katika mahojiano yake na BET, Ne-Yo amesema kwamba wimbo wa "Do You" ni sehemu ya pili ya wimbo wake wa awali wa "So Sick" ambao unatoka katika albamu yake ya kwanza ya In My Own Words.[1]

Remix ya wimbo huu amemshirikisha mwanamama Mary J. Blige. Na remix yake nyingine amepata kumshirikisha mwanadada mwingine aitwaye Hikaru Utada, ambao ulitolewa nchini Japan kunako 21 Novemba 2007 ikiwa kama mmoja kati ya wimbo wa 7 kwa tungo zake za Kiingereza kutoka kwa mwanadada huyo.

Video yake[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni kabisa Ne-Yo anaonekana akipigana na mpenzi wake wa zamani katika gari, ambaye baadaye aliondoka zake. Ne-Yo akawa anajaribu kuandika barua kwa mpenzi wake huyo huku akiwa anajaribu kumwuliza kama ana mkumbuka.

Inaonekana kuwa ni vigumu kwa yeye kumkumbuka, na baadaye akapata kusoma barua aliyotumiwa na Ne-Yo na akaamua kuikunja-kunja na kuitupilia mbali. Mpenzi huyo baada ya muda anaonekana kumpiga busu mpenzi wake mpya wakiwa katika kochi, na akiwa amemlalia mapajani, wakati huohuo akiwa amemkalia mbali kidogo.

Ne-Yo kisha akakumbuka sehemu ambayo alikuwa ana kawaida ya kumpiga busu mpenzi wake huyo katika kochi hilohilo alilokaa na huyo bwana mpya. Ne-Yo akaonekana akiendesha gari kwa kasi kisha akalisimamisha katika eneo lenye kibanda cha kupigia simu za kulipia, na kuanza kumpigia simu mpenzi wake wa zamani aje katika eno lile la kibanda cha simu za kulipia. Lakini kwa kwa bahati mbaya ule muda ambao dada yeye kafika, Ne-Yo yeye akawa tayari kesha ondoka zake.

Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (2007) Nafasik
Iliyoshika
Brazil Hot 100 14
U.S. Billboard Hot 100 26
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs 3
U.S. Billboard Pop 100 86
Official UK Singles Chart 100 [2]

Remix aliyoimba na Hikaru Utada[hariri | hariri chanzo]

Mauzo ya Digital na Chati za Ujapani[hariri | hariri chanzo]

Chati Nafasi
iliyoshika
Nyimbo za iTunes za Ujapani #1
Recochoku Chaku-Uta Downloads[3] #1
Recochoku Chaku-Uta Full[4] #1

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]