Didake
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Didake (yaani Mafundisho) ya Mitume Kumi na Wawili ni kimojawapo kati ya vitabu vya kale zaidi vya Ukristo, ambavyo viliandikwa na Mababu wa Kanisa na vinapatikana nje ya Biblia.
Kinakadiriwa kiliandikwa kati ya mwaka 70 na 150 BK katika mazingira ya Syria. Mwandishi wake hajulikani.
Kitabu kilipatikana tena mwaka 1873 huko Yerusalemu.
Lengo lake ni malezi ya Kikristo, yaani kupokeza mafundisho ya Mitume kwa katekesi juu ya maadili inayotofautisha "njia ya mauti" na "njia ya uzima", ikiwa na orodha ya vilema na maadili mema, ikifuatwa na matini ya liturujia na taratibu kuhusu ubatizo na ekaristi.
[hariri] Tafsiri ya Kiswahili
- Didakè yaani Mafundisho ya Mitume Kumi na Wawili na Waraka wa Mt. Klementi kwa Wakorinto, tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna (Italia) 1990 – ISBN 88-307-0321-4
[hariri] Marejeo
- Audet, Jean-Paul, La Didache, Instructions des Apôtres, J. Gabalda & Co., 1958.
- Draper, Jonathan, ed. 1996. The Didache in Modern Research (Leiden, New York and Cologne)
- Holmes, Michael W., ed., The Apostolic Fathers: Greek Texts and English Translations, Baker Academic, December 1, 1999. ISBN 978-0-8010-2225-8
- Lightfoot, Joseph Barber, et al., Apostolic Fathers, London: Macmillan and Co. 1889.
[hariri] Viungo vya nje
- CCEL Greek text
- Original Greek text
- Greek text (Roman transliteration)
- Early Christian Writings: Didache
- Catholic Encyclopedia 1908: Didache Source of some of the above text
- Jewish Encyclopedia: Didache
- Garrow on the Didache
- Didache translated by Richardson, Cyril C.
- Didache translated by Charles H. Hoole. - English translation hosted by about.com
- didache.info
- earlychurch.org.uk
- CCEL: Teaching of the Twelve Apostles
- upenn.edu
- Didache translated by Schaff
- Didache, The in the 1911 Encyclopædia Britannica
- Restoring the Beauty of the Didache, Zdziarski
- The DIDACHE or DUAE VIAE : the handbook of instructions of some early pneumatic Jewish Christians