Detepwani (familia)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Detepwani)
| Detepwani | ||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Detepwani ni ndege wa nusufamilia Cerylinae katika familia Alcedinidae. Spishi kubwa zinaitwa mkumburu. Wanafanana na midiria lakini spishi nyingi ni wakubwa zaidi na zote zina kishungi. Kwa kweli baina ya spishi hizi kuna zile kubwa kabisa za familia hii, lakini American pygmy kingfisher ni mdogo sana. Takriban spishi zote zina rangi ya majani ya metali mgongoni na nyekundu kidarini, lakini detepwani wa kawaida ni mweusi na mweupe tu.
Detepwani wamebobea kwa kukamata samaki lakini hula gegereka, vyura na wadudu pia. Huchimba tundu katika ukingo wa mto ambalo ndani lake jike huyataga mayai 2-5.
Spishi za Afrika [hariri]
- Ceryle rudis, Detepwani (Pied Kingfisher)
- Megaceryle maxima Mkumburu (Giant Kingfisher)
Spishi za mabara mengine [hariri]
- Chloroceryle aenea (American Pygmy Kingfisher)
- Chloroceryle amazona (Amazon Kingfisher)
- Chloroceryle americana (Green Kingfisher)
- Chloroceryle inda (Green-and-rufous Kingfisher)
- Megaceryle alcyon (Belted Kingfisher)
- Megaceryle lugubris (Crested Kingfisher)
- Megaceryle torquata (Ringed Kingfisher)