Desperate Housewives
| Desperate Hoisewives | |
|---|---|
![]() Nembo ya Desperate Housewives |
|
| Aina | Vichekesho |
| Imetungwa na | Marc Cherry |
| Nchi inayotoka | Marekani |
| Lugha | Kiingereza |
| Ina misimu | 7 |
| Utayarishaji | |
| Watayarishaji wakuu |
Marc Cherry Tom Spezialy (seasons 1-2) Michael Edelstein (seasons 1-2) Joe Keenan (season 3) George W. Perkins (seasons 3-4) Bob Daily (season 4) John Pardee & Joey Murphy (season 4) Kevin Murphy (co-exec) Chris Black (co-exec, season 2) Larry Shaw (co-exec, season 3) David Grossman (co-exec, season 3) |
| Muda | makisio ni dk. 43 |
| Urushaji wa matangazo | |
| Kituo | ABC |
| Viungo vya nje | |
Desperate Housewives ni kipindi cha Marekani kilichotungwa na Marc Cherry na kutayarishwa na ABC Studios pamoja na Marc CHerry Productions. Watayarishaji wakuu tangu msimu wa nne ni Marc Cherry, Bob Daily, George W. Perkins, John Pardee, Joey Murphy, David Grossman, Larry Shaw na Sabrina Wind.
Kipindi hiki kinawashirikishwa waigizaji wafuatao: Teri Hatcher kama Susan Mayer, Felicity Huffman kama Lynette Scavo, Marcia Cross kama Bree Van de Kamp na Eva Longoria Parker kama Gabrielle Solis. Brenda Strong ndiye muelezaji hadithi.
Tangu ilipoanza kwenye stesheni ya ABC mnamo Oktoba 3, 2004, kipindi hiki kimepata sifa nzuri kuotka watazamaji. Imeshinda tuzo zza Emmy Award na Golden Globe Award na tangu Aprili 2007, iliripotiwa kuwa kipindi kilicho maarufu zaidi kulingana na namba ya watazamaji kote duniani, ikiwa na watazamaji takriban milioni 120.[1]
Yaliyomo |
[hariri] Misimu
[hariri] Msimu wa kwanza
Desperate Housewives ilianza kuonyeshwa mnamo Oktoba 3, 2004 na inahusu watu wanne wakuu: Susan Mayer, Lynette Scavo, Bree Van de Kamp na Gabrielle Solis, pamoja na familia zao na majirani walioko kwenye barabara ya Wisteria Lane. Mada kuu ya msimu huu ni kujiua kwa Mary Alice Young. Bree anapigania kuokoa ndoa yake, Lynette anajitahidi kulea watoto wake watukutu, Susan anashindana na Edie ili kupata mapenzi ya Mike, na Gabrielle anajaribu kuficha uhusiano wake wa kando na John. Msimu huu unaisha pindi watu wote wanaamini kuwa Bree amempa sumu na kumuua mumewe, Carlos kujulushwa kuhusu uhusiano wa kando wa Gaby kabla ya yeye (Carlos) kupelekwa jela.
[hariri] Msimu wa pili
Ilianza mnamo Septemba 25, 2005 na mada yake kuu ni kuhusu jirani mpya aliyehamia Wisteria Lane saa sita za usiku. Katika msimu huu, Bree anajitahidi na maisha ya kuwa mjane, na hatimaye anaanza kulewa. Mtalaka wa Susan anapendana na Edie, na Lynette anapata kazi nzuri na kuwa meneja wa mumewe na Gabrielle anawacha mipango yake ya kando na ana azma ya kuwa na mimba ili kuanza familia. Inapoisha, Mike anagongwa na gari na Orson - ambaye atakuwa mumewe Bree kwenye msimu ujao.
[hariri] Msimu wa tatu
Ilianza Septemba 24, 2006. Bree anaolewa na Orson. Vilevile, Lynette anajitahidi kukabiliana na mwana wa kando wa mumewe. Tom anafungua mkahawa unaozidisha mzozo kati yake na mkewe. Gabrielle anawachana na mumewe na kupendana na Meya wa Fairview. Edie bado anamshawishi Mike kimapenzi. Susan naye anapendana na Muingereza mmoja aliye na mkewe mgonjwa mahututi.
[hariri] Msimu wa nne
Ilianza Septemba 30, 1997,[2] na mada yake kuu ni kuhusu Katherine Mayfair na familia yake. Hata hivyo, Lynette anakabiliana na saratani; Gabrielle, aliyeolewa na Meya, anaanza mpango wa kando na mtalaka wake Carlos; Susan na Mike wanafurahia maisha yao kama maharusi. Mashoga wawili wanaguria Wisteria Lane - Lee na Bob. Upepo mkali unakuja na kuvunja nyumba zote kwenye barabara ya Wisteria Lane.
[hariri] Msimu wa tano
Ilianza mnamo Septemba 28, 2008. Mada kuu ni kuhusu mumewe Edie Britt anayeitwa Dave Williams. Dave anataka kulipiza kisasi kwa mtu anayeishi Wisteria Lane. Lynette na Tom wanagundua kuwa mwana wao anapendana na mwanamke aliyeolewa. Carlos na Gabrielle wanakabiliana na watoto wawili: Juanita na Celia. Bree na Orson wanapata tabu kwenye ndoa yao. Orson anaanza tabia ya kuiba kutoka kwa majirani.
[hariri] Msimu wa sita
Ilianza Jumapili, Septemba 27, 2009 saa tatu jioni.[3] Mada kuu ni kuhusu mpango wa kando wa bree na Karl. Vipindi vilivyobaki 13 vitaendelea mnamo Januari 3, 2010.
[hariri] Wahusika Wakuu
- Teri Hatcher aliigiza kama Susan Mayer, mama aliyetalikiwa na angali akitafuta mpenzi.
- Felicity Huffman aliigiza kama Lynette Scavo, mama wa watoto wanne.
- Marcia Cross aliigiza kama Bree Van de Kamp
- Eva Longoria Parker aliigiza kama Gabrielle Solis, ambaye ni mwanamitindo na aliyeanza mpango wa kando na kijana wa miaka 17.
- Nicollette Sheridan aliigiza kama Edie Britt, adui wa Susan.
- Ricardo Antonio Chavira aliigiza kama mumewe Gabrielle, aitwaye Carlos Solis.
- James Denton aliigiza kama Mike Delfino, mpenzi wa Susan.
- Doug Savant aliigiza kama Tom Scavo, mumewe Lynette.
[hariri] Mafanikio
| Msimu | Saa | Mwanzo wa msimu | Mwisho wa msimu | Msimu wote | Namba | Watazamaji (milioni) |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Sunday 9:00 P.M. | Oktoba 4, 2004 | Mei 22, 2005 | 2004-2005 | #4[4] | 23.8[4] |
| 2 | Sunday 9:00 P.M. | Septemba 25, 2005 | Mei 21, 2006 | 2005-2006 | #4[5] | 21.7[5] |
| 3 | Sunday 9:00 P.M. | Septemba 24, 2006 | Mei 20, 2007 | 2006-2007 | #10[6] | 17.5[6] |
| 4 | Sunday 9:00 P.M. | Septemba 30, 2007 | Mei 18, 2008 | 2007-2008 | #6[7] | 18.6[7] |
| 5 | Sunday 9:00 P.M. | Septemba 28, 2008 | Mei 17, 2009 | 2008-2009 | #9[8] | 15.6[8] |
| 6 | Sunday 9:00 P.M. | Septemba 27, 2009 | Mei 2010 | 2009-2010 | #20 | 14.9 |
[hariri] Tuzo
- Mnamo 2006, kipindi hiki kilipata tuzo ya Golden Globe for Best TV Musical or Comedy Series.
- Mnamo 2005, ilishinda tuzo la People's Choice Award for Favorite New Television Drama.[9]
[hariri] Marejeo
- ↑ Desperate Housewives On SABC3 Confirmed, TVSA News Desk, April 3, 2007
- ↑ ABC Announces Fall Première Dates, The Futon Critic, July 25, 2007
- ↑ ABC Announces Fall Premiere Dates for 19 Shows. TVGuide.com. Rudishwa juu ya 2009-06-09.
- ↑ 4.0 4.1 Season Program Rankings from 09/20/04 through 05/22/05. ABC Medianet (May 24, 2005). Rudishwa juu ya 2009-07-03.
- ↑ 5.0 5.1 Season Program Rankings from 09/19/05 through 05/28/06. ABC Medianet (May 28, 2006). Rudishwa juu ya 2009-07-03.
- ↑ 6.0 6.1 Season Program Rankings from 09/18/06 through 06/03/07. ABC Medianet (June 3, 2007). Rudishwa juu ya 2009-07-03.
- ↑ 7.0 7.1 Season Program Rankings from 09/24/07 through 05/25/08. ABC Medianet (May 28, 2008). Rudishwa juu ya 2009-07-03.
- ↑ 8.0 8.1 Season Program Rankings from 09/22/08 through 05/17/09. ABC Medianet (May 19, 2009). Rudishwa juu ya 2009-07-03.
- ↑ The IMDb.com list of awards for Desperate Housewives, Retrieved August 3, 2007
