Dear Mama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Dear Mama”
“Dear Mama” cover
Single ya 2Pac
kutoka katika albamu ya Me Against the World
Imetolewa 21 Februari 1995
Muundo 12", Cassette, CD, Maxi
Imerekodiwa 1994
Aina Hip hop, ballad, R&B
Urefu 4:39
Studio Interscope
Mtunzi T. Shakur, J. Sample, T. Pizarro
Mtayarishaji Tony Pizarro, DF Master Tee (mtayarishaji-mwenza), Moses (co-producer)
Certification Platinum (RIAA)
Mwenendo wa single za 2Pac
"Holla If Ya Hear Me"
(1993)
"Dear Mama"
(1995)
"So Many Tears"
(1995)

"Dear Mama" ni wimbo wa rap ulioimbwa na msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani, 2Pac. Wimbo ulitayarishwa na Tony Pizarro kwa ajili ya albamu ya tatu ya 2Pac Me Against the World, iliyotolewa mnamo 1995. "Dear Mama" ulitungwa na 2Pac kwa ajili ya mama'ke mwenyewe, Afeni Shakur.

"Dear Mama" ulitolewa mnamo tar. 21 Februari 1995 ukiwa kama single ya kwanza kutoka katika albamu. Single hii ilikuwa moja kati ya single zilizopata mafanikio makubwa sana kupita zote zilizotoka kwenye albamu ya Me Against the World. Wimb huu huhesabiwa na watahakiki, mashabiki, na wenye kusisitiza usafaha ikiwa kama moja kati vibao vikali vya hip hop vya muda wote, na kimsingi ni miongoni mwa nyimbo bab-kubwa za 2Pac, kwa kupewa nafasi ya nne kwenye orodha Nyimbo Bora 100 za Rap za About.com.[1]

Uhakiki na mafanikio kibiashara[hariri | hariri chanzo]

Wimbo ulichukua nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot Rap Singles kwa takriban majuma matano, kwenye R&B/Hip-Hop Singles ulikaa kwa juma moja, na kushika nafasi ya #9 kwenye chati za Hot 100. Pia ilikaa nafasi ya juu kwenye chati za mauzo ya Hot Dance Music Maxi-Singles kwa takriban majuma manne. Single hii ilitunukiwa Platinum na RIAA mnamo tar. 13 Julai 1995.[2]

Huhesabiwa na wengi kuwa ni kibao cha huzuni zaidi cha 2Pac pia wimbo wenye kuheshiwa sana, na umepata kusifiwa na wasanii wengi tu (Eminem ametaja kama ni wimbo wake kipenzi)[3], tena hata na wasanii wengi ambao hawajihusishi na masuala ya hip hop nao wameusifu. Mnamo 1998, wimbo umeonekana kwenye albamu vya Vibao Vikali vya Tupac. Toleo la pili la wimbo huu ulitayarishwa na Nitty akishirikiana na Anthony Hamilton kwenye toleo la albamu ya Tupac ya 2006, Pac's Life.

Snoop Dogg alisema kwenye mahojiano kwamba kibao hiki kimeonesha upande kamili wa hisia za 2Pac, ambapo imemfanya kuwa tofauti na marapa wengine, kwa sababu "amezama ndani sana", kitu ambacho marapa wengine huwa wanasita au hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Wimbo umeonekana kwenye Mfululizo wa FOX New York Undercover.

Muziki wa video[hariri | hariri chanzo]

Muziki wa video wa "Dear Mama" uliongozwa na Calvin Caday wakati 2Pac kafungwa; hivyo basi, ameonekana kuwa na mazoea ya wakati wa kama huo kwenye video kwa Tupac. Afeni Shakur pia alishirikishwa, ameonekana kupitia kurasa zilizorushwa za albamu ya picha iliokuwa ikizunguka na kumwonesha picha ya Tupac wakati yungali bwana mdogo. Video pia imeonesha makala fupi inayohusiana na Black Panthers, inadokezea historia yake ya awali kwamba alikuwa mwanachama wa jumuia ya kisiasa.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

12", Cassette, CD, Maxi[4]
  1. "Dear Mama" (LP Version) — 4:41
  2. "Dear Mama" (Instrumental) — 5:21
  3. "Bury Me a G" — 4:59
  4. "Dear Mama" (Moe Z. Mix) — 5:09
  5. "Dear Mama" (Instrumental Moe Z. Mix) — 5:09
  6. "Old School" (LP Version) — 4:59

Chati zake[hariri | hariri chanzo]

Chati (1995)[5] Nafasi
iliyoshika
U.S. Billboard Hot 100 9
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks 3
U.S. Billboard Hot Rap Singles 1
UK Singles Chart 27
RIANZ New Zealand Singles Chart 4

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Adaso, Henry. About.com: Rap/Hip-Hop: 100 Greatest Rap Songs. About.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-04-05. Iliwekwa mnamo 2008-02-17.
  2. RIAA Gold & Platinum Searchable Database - Platinum Singles, riaa.com, Accessed 3 Julai 2009
  3. Tupac: Resurrection
  4. Dear Mama (US Single #1) at Allmusic. Allmusic. Iliwekwa mnamo 2009-04-17.
  5. Me Against the World: Billboard Singles. Allmusic. Iliwekwa mnamo 2009-04-17.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]