David Munyasia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
David Munyasia

David Munyasia ni bondia wa Kenya, wa kwanza kupatikana na makosa ya kuvunja kanuni za Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya kutotumia visisimua misuli, wakati wa mashindano ya Olimpiki ya 2004 kule Athens.

Mnamo Agosti 10, 2004, Kamati hiyo ilitangaza kuwa Munyasia, bondia wa Bantamweight amepimwa na kudhihirika kuwa alikuwa ametumia miadarati ya Cathine mnamo Agosti 6. Alipatikana na kiwango mara nne cha kili cha juu zaidi kinachokubalika cha maikrogramu 5 kwa miliilita moja katika mkojo wake. Papo hapo alikataliwa kushiriki katika mashindano hayo. Munyasia alikiri kuwa alikuwa akitumia miraa (qat), kisisimua misuli maarufu nchini Kenya.

Mwaka mmoja awali, alikuwa ameshinda nishani ya Fedha katika Mashindano ya All-Africa, uzani wa Bantamweight, jijini Abuja, Nigeria. Alifuzu katika mashindano ya Olimpiki ya Athens kwa kushinda nishani ya Shaba katika mashindano ya 1st AIBA African 2004 Olympic Qualifying Tournament jijini Casablanca, Morocco. Katika pigano la mwisho alishindwa na Mohamed Abdelsayed wa Egypt.

Marufuku yake iliisha mwaka wa 2006 na anatarajiwa kurudi ulingoni[1].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Habari kumhusu Bondia David Munyasia East African Standard

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]