D'banj

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
D'banj
D'banjawards.jpg
Maelezo ya awali

Dapo Daniel Oyebanjo (amezaliwa mwaka 1980 Zaria, Jimbo la Kaduna, Nigeria), anajulikana kama, D'banj ni mtunzi na mwimbaji kutoka Nigeria. "Dapo" ni ufupi wa jina la Kiyoruba "Ifedapo" (maana "Upendo ulikuja pamoja"). [1]

Yaliyomo

Wasifu [hariri]

Maisha Yake ya Utotoni [hariri]

D'banj alizaliwa na afisa wa vifaa vya vita ambaye alikuwa amefanikiwa na ambaye aliongoza kundi lake na hata kuna barabara lililopewa jina lake katika makao ya jeshi ya Alamala, Abeokuta, na mama wa kanisa, aliyetoka Shagamu katika Jimbo la Ogun. Kutokana na taaluma ya baba yake, yeye alihamia mara kadhaa ndani ya Nigeria na pia walihamia India. D'banj pia alitarajiwa kufuata kazi ya baba yake ya kijeshi na alikuwa ajiunge na Shule ya Jeshi ya Nigeria, Zaria akiwa na umri wa miaka kumi na moja.[2]

Mwanzo wa Muziki [hariri]

D'banj alilelewa akisikiliza Fela Kuti, ambaye anamkumbuka kama "mshauri mkuu" wake.[3]. Yeye alijulishwa kucheza filimbi kwa marehemu kakake, Femi Oyebanjo, ambaye alikufa katika ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka kumi na saba.[2] Kwa vile upendo wa D'banj wa muziki ulikuwa mkubwa kuliko matarajio ya kijeshi ya wazazi wake, ilikuwa vigumu kupata idhini ya wazazi wake; hii inaweza kupatikana vema kupitia wimbo wake, All Da Way kutoka albamu yake ya kwanza. Alitoa jina lake la kisanii kutoka mseto ya jina lake la kwanza na la kati.

Wasifu wa Muziki [hariri]

Kama heshima kwa mshauri wake, Fela, D'banj alirudisha muziki aina ya Afrobeat katika karne ya 21 vilevile akiitia dawa nzuri ya ucheshi. Nyimbo yake zina msingi ya maisha yake, mara nyingi huchekesha lakini pia zina maana ya ndani ambayo huashiria mapambano ya vijana wa Afrika kujaribu kufikia ndoto zao. Yeye huimba katika Yoruba, Kiingereza na Kiingereza aina ya Pidgin . Albamu zake zote zimetayarishwa na Don Jazzy na yeye mwenyewe.

2005-2006: No Long Thing [hariri]

Albamu ya kwanza ya D'banj, No Long Thing, ilitolewa mwaka 2005, ikiwa na nyimbo kadhaa, pamoja na Tongolo kama wimbo maarufu. Hii ilionekana kuwa wimbo wa kumpatia ustawi na umaarufu. Pia ilimpatia ubinafsi wa Koko Master neno Koko likiwa na maana kadhaa. Mafanikio ya D'banj yaliwezesha mashirikiano na wasanii wawili, kama vile katika albamu ya Dare Art-Alade, kuna wimbo ya escalade Part 2 na pia wimbo katika albamu ya Ikechukwu, uitwao Doo.

2007: Rundown Funk U Up [hariri]

Albamu ya pili ya D'banj Rundown Funk U Up, ambayo ilitolewa mwaka 2006, ilikuwa na nyimbo kadhaa ikiwa ni pamoja na Tongolo (Remix) na wimbo moja maarufu, Mbona Mimi?. Hii ilipata mafanikio zaidi.

2007-2008: Curriculum Vitae na The Entertainer [hariri]

D'banj, kama mwanasanaa ya Mo 'Hits Records, pia ni mwanachama wa kundi la Mo' Hits Allstars. Yeye mara kwa mara ameonekana miongoni mwa wenye vipaji vya kuimba kama vile, "Smile Lasisi". Ya pamoja albamu ya kwanza, Curriculum Vitae, ilitolewa katika Desemba 2008. Ni pamoja na wimbo wake maarufu, Be Close To You, Booty Call na Move Your Body, ambayo ilikuwa wimbo maarufu. D'banj alishiriki katika wimbo wa Ikechukwu wa 2008, Wind Am Well. Julai 2008 D'banj alitoa albamu yake ya tatu, The Entertainer [4] pamoja na wimbo Gbono Feli Feli, Kimon, Ọlọrun Maje na Entertainer.

2009 [hariri]

Aliitwa Michael Jackson wa Afrika na Wyclef walipokutana katika MTV AFRICAN MUSIC AWARDS 2009.

Akiwa kwenye Ukumbi [hariri]

D'banj anajulikana mwigizaji mwenye nguvu, na jitihada. Kwa kawaida yeye huigiza katika sherehe ya muziki ya ThisDay Africa Rising. Ameimba katika sherehe ya Femi Kuti iitwayo new Afrikan Shrine mjini Lagos vilevile katika sherehe ya Shrine Synchro System's Regular London Night katika Cargo. Yeye pia kutumbuiza katika sherehe ya Black President katika kumbukumbu ya sanaa ya Fela katika Barbican jijini London. Pia aliimba pamoja na wasanii wengi wa kimataifa kama Kelly Rowland katika Toleo la kwanza la MTV Africa Music Awards 2009 katika Abuja, Nigeria. Alikuwa pia akishiriki katika mojawapo ya sherehe zilizo tarajiwa zaidi 'Koko Concert'. Sherehe hii ilikuwa na D'Banj, Don Jazzy, Dr SID, Wande Coal, D'Prince, na Mo Hits Ikechukwu pamoja na wasanii kama May7ven na mchekeshi Tunde Ednut. Ukumbi uliandaliwa kwa usiku wa kutumbuiza - athari za Koko zilionekana wazi jijini London kwani mashabiki wa D'banj na Mo'Hits walijaza uwanja huo kabisa. Kama ilivyotarajiwa, nyimbo zuri ziliimbwa na kasi na shauku ya mashabiki ilidumishwa na wasanii wenyewe jukwaani. D'banj pia ni moja ya wanamuziki waliopendwa sana Nigeria. Utendaji wake wakati katika Star mega Jamz ulikuwa d-bomb. - Petmee [5]

Kazi ya Utu [hariri]

D'banj ni mwanzilishi wa shirika la vijana la Koko la kuendeleza amani Yeye pia ni wa balozi wa kwanza kutoka Nigeria vijana wa Umoja wa Mataifa wa Amani.[6]

Binafsi Usalama / ASASI [hariri]

Mlinzi binafsi wa D'banj ni mtu mwenye mafunzo ya kijeshi kwa jina la Isaka Ekpo.

Diskografia [hariri]

Albamu [hariri]

Nyimbo Zake [hariri]

  • Tongolo (2005)
  • Socor (2005)
  • Mobolowowon (2005)
  • Run Down (2006)
  • Why Me (2006)
  • Move Your Body (akimshirikisha Wande Coal) (2007)
  • Kimon (2008)
  • Ọlọrun Maje (2008)
  • Gbono Fele (2008)
  • Entertainer (2008)
  • Suddenly (2008)
  • Fall In Love (2008)
  • Igwe (2008)

Nyimbo alizoshirikishwa [hariri]

  • Wind Am Well (akimshirikisha Don Ikechukwu Jazzy na D'banj) (2008)

Tuzo [hariri]

Alishinda

Ameteuliwa:

Angalia Pia [hariri]

Marejeo [hariri]

Viungo vya nje [hariri]