Ucheki
|
|||||
| Wito la taifa: Pravda vítězí (Kicheki: "Ukweli hushinda") |
|||||
| Wimbo wa taifa: Kde domov můj | |||||
| Mji mkuu | Praha |
||||
| Mji mkubwa nchini | Praha | ||||
| Lugha rasmi | Kicheki | ||||
| Serikali | Jamhuri Miloš Zeman Petr Nečas |
||||
| ' Kutokea kwa taifa Uhuru kutoka Austria-Hungaria Mwisho wa Chekoslovakia |
Karne ya 9 (Dola la Moravia) 28 Oktoba 1918 1 Januari 1993 |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
78,866 km² (ya 117) 2.0 |
||||
| Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
10,265,231 (ya 78) 10,230,060 130/km² (ya 77) |
||||
| Fedha | Koruna (CZK) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
| Intaneti TLD | .cz 3 | ||||
| Kodi ya simu | +4201
|
||||
Ucheki (Kicheki: Česko) pia Jamhuri ya Kicheki au Jamhuri ya Czech (Kicheki: Česká republika) ni nchi ya Ulaya ya Kati na mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Imepakana na Poland, Ujerumani, Austria na Slovakia. Mji mkuu ni Praha (Kijer.: Prag; Kiing.: Prague).
Miji mingine mikubwa ni Brno, Ostrava, Zlín, Plzeň, Pardubice, Hradec Králové, České Budějovice, Liberec, Olomouc na Ústí nad Labem.
Tangu zamani nchi imekuwa na kanda mbili za Bohemia, Moravia na Silesia.
Wakazi husema hasa Kicheki ambacho ni lugha ya Kislavoni ya Magharibi.
Historia [hariri]
Historia ya jamuhuri ya Cheki yenyewe si refu, tukiangalia tangu nchi hiyo kupokea uhuru kamili, mwaka wa 1993 hadi leo. hapo awali Cheki ilikuwa imeungana na Slovakia wakiwa Cheko-slovakia Czechoslovakia Chekoslovakia ilikuwa chini ya utawala wa ufalme wa Austro-Hungarian katika karne ya 19 na 20. mapema zaidi ufalme wa Moravia kuu katika karne ya 7. walitawaliwa mpaka vita kuu ya kwanza ya dunia wakati ufalme ulianguka, wakawa na nchi huru ya cheko-slovakia. Rais wa kwanza kuteuliwa kwa taifa hilo mpya ni Tomas Garrigue Masaryk. wakati wa vita kuu ya pili ya dunia wajerumani walichukuwa uongozi wa Chekoslovakia. hawaku dumu mno. Kufikia mwisho wa vita huo USSR ilichukuwa nahodha nakuweka nchi hio katika sera ya kikomunisti. walitawaliwa kwa nguvu halisi hadi mwaka wa 1989 wakati kulitokea mapenduzi ya kiamani na kupata uhuru wake rasmi na demokrasia. mwaka wa 1993, nchi hio iligawanyika katika Cheki na Slovakia kwasababu ya kisiasa. mwaka wa 1999 nchi ya Cheki ilijiunga na NATO. cheki imekuwa mwanachama wa muungano ya Umoja wa Ulaya kuanzia mwaka wa 2004. Cheki nimaarufu katika dunia kwa usalama wake na inapendwa sana na mamilioni ya watalii ambao huizuru kila.
Viungo vya nje [hariri]
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ucheki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
|
||||||||||||||