Cuba Gooding, Jr.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cuba Gooding, Jr.

Gooding, Jr. mnamo Aprili 2022
Amezaliwa Cuba M. Gooding, Jr.
2 Januari 1968 (1968-01-02) (umri 56)
Kazi yake Mwigizaji/Mtayarishaji filamu
Miaka ya kazi 1987–mpaka sasa
Ndoa Sara Kapfer (13 Machi 1994) watoto wa 3

Cuba M. Gooding, Jr. (amezaliwa tar. 12 Januari 1968) ni mwigizaji filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika sana kwa ushindi wake Tuzo ya Academy-akiwa kama mwigizaji mwandamizi bora kwenye filamu ya Jerry Maguire ambamo kacheza kama Rod Tidwell mnamo 1996, akiwa sambamba kabisa na Tom Cruise. Pia anafahamika sana kwa kucheza kwenye filamu iliongozwa na John Singleton ya Boyz n the Hood mnamo mwaka wa 1991.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Cuba Gooding, Jr. alizaliwa na kukulia mjini The Bronx, New York, akiwa kama mtoto wa Shirley, mwimbaji mwenye sauti Nyororo, na Cuba Gooding, Sr., mwimbaji kiongozi wa kundi la muziki wa soul la The Main Ingredient.[1] Ana ndugu wa kiume wawili, mwanamuziki Tommy Gooding na mwigizaji mwenzi wake Omar Gooding. Familia yake ilihamia mjini Los Angeles baada ya kundi la Mzee wake kupata kibao chao kikali "Everybody Plays the Fool" mnamo mwaka wa 1972; halafu mzee wake akajitia kuitelekeza familia yake baada ya miaka miwili baadaye. Wakati wa kuonekana kwake kwenye Baada ya kuonekana kwake kwenye The Howard Stern Show, Gooding akagundua kwamba baada ya baba yake kuondoka, familia yake ilikuwa ikiishi kwenye mahoteli kila kukicha huko mjini Los Angeles. Gooding alililewa na mama yake na kuhudhuria kwenye mashule tofauti takriban mane: North Hollywood High School, Tustin High School, Apple Valley High School, na John F. Kennedy High School ya mjini Granada Hills huko Los Angeles. Alipata kutumikia kama rais kwenye mashule hayo tofauti matatu. Amekuwa muumini wa dhehebu la Born again akiwa na umri wa miaka takriban 13.[2]

Shughuli za uigizaji[hariri | hariri chanzo]

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Filamu Uhusika Maelezo mengine
1988 Coming to America Barber Shop Customer
1989 Judgement Officer Alvarez
Sing Stanley
1991 Boyz n the Hood Tré Styles
1992 Gladiator Abraham Lincoln Haines
A Few Good Men Cpl. Carl Hammaker
1993 Daybreak Torch (Stephen Tolkin)
Judgment Night Mike Peterson
1994 Lightning Jack Ben Doyle
1995 Outbreak Maj. Salt
The Tuskegee Airmen Billy Roberts
Losing Isaiah Eddie Hughes
1996 Jerry Maguire Rod Tidwell Kashinda Tuzo ya Academy akiwa kama Mwigizaji-Mwandamizi Bora
Kateuliwa— Golden Globe
1997 As Good as It Gets Frank Sachs
Do Me a Favor Liquor Store Clerk
1998 What Dreams Mei Come Albert Lewis
A Murder of Crows Lawson Russel Imetayarishwa na Derek Broes
1999 Instinct Theo Caulder
Chill Factor Arlo
2000 Men of Honor BM2/Chief/Senior Chief Carl Brashear
2001 Pearl Harbor Petty Officer Doris Miller
Rat Race Owen Templeton
Zoolander Himself
In the Shadows Draven
2002 Snow Dogs Theodore "Ted" Brooks
2003 Boat Trip Jerry Robinson
The Fighting Temptations Darrin Hill
Radio James Robert "Radio" Kennedy
2004 Home on the Range Buck voice-over
2005 Dirty Salim Adel
Shadowboxer Mikey
2006 End Game Alex Thomas
Lightfield's Home Videos
2007 Norbit Deion Hughes
What Love Is Tom
Daddy Day Camp Charlie Hinton
American Gangster Leroy Barnes
The Land Before Time XIII: The Wisdom of Friends Loofah voice-over
2008 Hero Wanted Liam Case
Harold Cromer
Linewatch Michael Dixon
The Way of War David Wolfe
2009 Gifted Hands: The Ben Carson Story Ben Carson TV film
Lies & Illusions Isaac
The Devil's Tomb Mack
Wrong Turn At Tahoe Joshua
Hardwired[3] Luke Gibson
2010 Wrong Side of Town Clay Freeman
Red Tails TBA

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Gaul, Lou (7 Agosti 2008). Cuba Gooding Jr. talks 'Daddy Day Camp'. 'Phillyburbs'. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-02-20. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2009.
  2. Williams, Kam (15 Agosti 2007). Cuba Gooding: The Daddy Day Camp Interview with Kam Williams. 'Kamwilliams'. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2009.
  3. http://www.imdb.com/title/tt1405412/

Viungo vy Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons