Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
|
|||||
| Wito la taifa: Justice - Paix - Travail (Kifaransa: "Haki - Amani - Kazi") |
|||||
| Wimbo wa taifa: Debout Congolais | |||||
| Mji mkuu | Kinshasa |
||||
| Mji mkubwa kushinda miji mingine yote |
Kinshasa | ||||
| Lugha rasmi | Kifaransa (Kingala, Kikongo, Kiswahili, Kiluba ni lugha ya taifa) | ||||
| Serikali
• Rais
|
Serikali ya mseto Joseph Kabila |
||||
| Uhuru - Tarehe |
Kutoka Ubelgiji 30 Juni 1960 |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
2,345,410 km² (12th) 3.3% |
||||
| Idadi ya watu - 2006 kadiriwa - 1938 census - Msongamano wa watu |
62,660,551 (20th) 10,217,408 24/km² (182nd) |
||||
| Fedha | Congolese franc (CDF) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET, EET (UTC+1 na +2) - (UTC+1 na +2) |
||||
| Intaneti TLD | .cd | ||||
| Kodi ya simu | +243 |
||||
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (au Kongo-Kinshasa) ni nchi iliyoko Afrika ya Kati; kwa ukubwa wa eneo ni ya pili barani Afrika. Ni tofauti na nchi jirani ya Jamhuri ya Kongo. Kati ya 1971 na 1997 nchi iliitwa "Zaire".
Yaliyomo |
Jiografia [hariri]
Nchi imepakana na Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi, Tanzania, Zambia na Angola. Ina sehemu ndogo iliyopakana na pwani ya Bahari ya Atlantiki. Sehemu hiyo inatenganisha eneo la Cabinda kutoka maeneo mengine ya Jamhuri ya Angola.
Historia [hariri]
Nchi jinsi ilivyo ilianzishwa kama koloni la Kongo ya Kibelgiji. Jina la Kongo lahusiana na mto Kongo unaopitia nchi yote na pia Ufalme wa Kongo uliopatikana zamani katika sehemu za magharibi za Angola na Kongo ya leo.
Upande wa kusini, kuanzia karne ya 17, kulikuwa na ufalme ulioitwa Dola la Kazembe.
Kati ya 27 Oktoba 1971 na 17 Mei 1997 nchi ilijulikana kwa jina la "Zaire".
Lualaba ni mkoa mpya wa Mashariki ya Congo-Zaire |
Mikoa [hariri]
Nchi imegawiwa kwa mikoa 11. Katiba mpya ilitarajia ugawaji kwa majimbo mapya 25 lakini kanuni hii haikutekelezwa na wakati wa Januari 2011 raisi alitangaza ya kwamba mipango ya ugawaji mpya imefutwa.
Lugha [hariri]
Kifaransa ni lugha rasmi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ilikuwa lugha ya utawala ya koloni ikaendelea kutumiwa kama lugha isiyoelekea upande wowote kati ya makabila, lugha na tamaduni za nchi hii. Lugha ya Kiholanzi iliyotumiwa na Wabelgiji pamoja na Kifaransa katika utawala haiko tena.
Kwa jumla kuna takriban lugha 242 zinazozungumzwa nchini (angalia orodha ya lugha). Lugha 4 zinatambuliwa kama lugha za kitaifa ambazo ni Kikongo (Kituba), Kingala, Kiluba (Tshiluba) na Kiswahili.
Kingala kilikuwa lugha rasmi ya jeshi la kikoloni liloitwa "Force Publique" chini ya utawala wa Ubelgiji likaendelea kuwa lugha ya jeshi la jamhuri baada ya uhuru.
Tangu mapinduzi ya 1997 sehemu za jeshi hasa katika mashariki hutumia pia Kiswahili.
Wakati wa ukoloni lugha nne za kitaifa ziliwahi kutumiwa kieneo katika shule za msingi.
Takriban watu 24,320,000 wanatumia Kifaransa kama lugha ya kwanza au ya pili.
Dini [hariri]
Wananchi karibu wote wanajihesabu Wakristo wa madhehebu mbalimbali; asilimia 50 hivi ni Wakatoliki.
Viungo vya nje [hariri]
- Uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia baada ya miongo minne
- Habari za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo toka BBC
| Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Nchi za Afrika | |
|---|---|
| Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
| Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
| Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia | |