Come On Over

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Come on Over”
“Come on Over” cover
Single ya Shania Twain
B-side "Man! I Feel Like a Woman!"

"Come on Over" ni wimbo ulioshinda katika Grammy Awardambao umeimbwa na mwimbaji kutoka Canada Shania Twain. Ilikuwa Single ya tisa kwa country adio na pia iliipa jia albamu yake ya 1999 Come on Over. Ulitungwa na Twain na aliyekuwa mumewe wakati huo, Mutt Lange. Ilitolewa mara ya kwanza kwa redio za Country za Amerika Kaskazini mwishoni mwa 1999. Wimbo huu ulinawili hadi kushinda tuzo la Grammy mnamo 2000.[1]. Baadaye wimbo huu ulishirikishwa katika albamu ya 2004 ya Twain Greatest Hits

Upokelezi wake[hariri | hariri chanzo]

Billboard magazine ilipokea wimbo huu kwa kuusifu huku wakiutaja kama ujumbe wa kuchangamsha uliotozwa ndani ya Muziki na wakngamua kuwa ungekuwa hit kwa siku zijazo[2]

Video[hariri | hariri chanzo]

Kanda ya Video ya Muziki kwa "Come on Over" ilichukuliwa kutoka katika DVD ya live ya 1999 ya Twain katika tamasha jijini Dallas. Ilitayarishwa mnamo 12 Septemba 1998 na kutolewa zaidi a mwaka mmoja baadaye mnamo 6 Oktoba 1999. Inaelekezwa na Larry Jordan. Hii ni video ya pili ya ‘’live’’ iliyotolewa kutoka albamu ya Come on Over kufuatia "Honey, I'm Home". Video iliyofuatia baada ya "Come on Over" ilikuwa "Rock This Country!" ambayo ilitolewa katika tamasha. Video hii inapatikana katika DVD ya Twain ya The Platinum Collection.

Unawili Katika Chati[hariri | hariri chanzo]

"Come on Over" iliingia katika chati ya Billboard Hot Country Singles & Tracks katika juma la 11 Septemba 1999 katika nafasi ya 52, Debut ya juu kabisa ya juma. Single hii ilikaa kwa chati kwa majuma 20 na ikapanda hadi kufikia #6 mnamo Mesemba 4, 1999, ambapo ilikaa kwa majuma mawili. "Come on Over" ilikuwa single ya nane katika kumi bora kutoka albamu ya Come on Over, single yake ya 12 kwa ujumla, na pia ya 15 katika single ishirini za juu. Katika Billboard Hot 100, ilifikia kilele katika nafasi ya 58 ingawa ilifika #43 katika chati ya Hot 100 Airplay. Nchini Canada, wimbo huu ulianzia #1 katika chati ya RPM Country Singles.[3].

Matoleo Rasmi[hariri | hariri chanzo]

  • Albamu ya Asili (2:55)
  • Toleo la Kimataifa (2:55)
  • Live from Dallas (3:00)

Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati[4] Kilele
Canadian Singles Chart 19
Canada RPM Country Singles 1
U.S. Billboard Hot Country Singles & Tracks 6
U.S. Billboard Hot 100 58

Vidokezo[hariri | hariri chanzo]

Alitanguliwa na
"Something Like That"
ya Tim McGraw
RPM Country Tracks
Single inayoongoza

1 Novemba-8 Novemba 1999
Akafuatiwa na
"I Love You"
by Martina McBride