Bundi (pia mabundi) ni ndege mbua wa familia Tytonidae na jenasi mbalimbali ya familia Strigidae. Ukurasa huu unahusu familia Strigidae. Spishi hizi zina kichwa kikubwa chenye umbo wa mviringo, mkia mfupi na rangi ya kamafleji. Kwa kawaida jike ni mkubwa kuliko dume. Mabawa yao ni marefu na mapana. Bundi hula ndege na wanyama wadogo, wanyama wagugunaji hasa, lakini watambaachi na wadudu wakubwa pia. Jike huyataga mayai 2-7 katika shimo ndani ya mti au tago lililoachwa na ndege mwingine, pengine katika sanduku la kutagia.
Bundi wengi huwinda usiku na hupumzika mchana. Walilenga windo lao kwa msaada ya masikio yao. Manyoya ya uso yapeleka mawimbi ya sauti kwa vipenyo vya masikio ambavyo kimoja kipo juu kidogo kuliko kingine. Hivyo waweza kulikamata windo bila kuliona. Windo hawezi kumsikia bundi akija, kwa sababu mabawa ya bundi hayafanyi sauti yo yote kwa kuwa kingo ya mbele ya manyoya ya mabawa imekerezekakerezeka na ile ya nyuma ina matamvua. Hii yapunguza vurugu ya hewa na kwa hivyo uvumi.
Spishi za Afrika [hariri]
Spishi za mabara mengine [hariri]
Spishi ya kabla ya historia [hariri]
- Asio brevipes (Mwisho wa Pliocene ya Hagerman, MMA)
- Asio priscus (Mwisho wa Pliocene ya Kisiwa cha Santa Rosa, MMA)
- Strix brea (mwisho wa Pleistocene ya Amerika ya Kaskazini)
- Strix dakota (mwanzo wa Miocene ya South Dakota, MMA) – labda haistahili kuwa katika jenasi Strix
- Strix edwardsi (kati ya Miocene ya Grive-Saint-Alban, Ufaransa) – labda yastahili kuwa katika jenasi Ninox
- Strix ignota (kati ya Miocene ya Sansan, Ufaransa) – labda haistahili kuwa katika jenasi Strix
- Strix intermedia (mwanzo – kati ya Pleistocene ya Ulaya ya Kati) – labda ni spishi ndogo ya S. Aluco ambayo imekwisha sasa
- Strix wintershofensis (mwanzo – kati ya Miocene ya Wintershof, Ujerumani wa Magharibi) – labda yastahili kuwa katika jenasi Ninox
- Strix sp. (mwisho wa Miocene ya Nebraska, MMA)
- Strix sp. (mwisho wa Pliocene ya Rębielice Królewski, Poland)
- Strix sp. (mwisho wa Pleistocene ya Ladds, MMA)