Fuko-dhahabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Chrysochloridae)
Rukia: urambazaji, tafuta
Fuko-dhahabu
Fuko-dhahabu asiyetambuliwa
Fuko-dhahabu asiyetambuliwa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Oda: Afrosoricida (Wanyama kama tandaraka
Nusuoda: Chrysochloridea (Wanyama kama fuko-dhahabu)
Familia: Chrysochloridae (Wanyama walio na mnasaba na fuko-dhahabu)
Gray, 1825
Ngazi za chini

Nusufamilia 2:
Amblysominae Simonetta, 1957
Chrysochlorinae Gray, 1825

Fuko-dhahabu au fuko butu ni wanyama wa familia Chrysochloridae ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama wengine waitwao fuko ni wanafamilia wa Bathyergidae na Spalacidae (oda Rodentia), Talpidae (Soricomorpha) na Notoryctidae (Notoryctemorphia). Spishi zote za fuko-dhahabu zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Hula wadudu. Fuko hawa huchimba mahandaki yao na miguu ya mbele iliyo na ukucha wa tatu ambao umevuvumulika. Vidole vya kwanza na vya nne vimebaki kama masalio na kile cha tano kimepotea. Miguu ya nyuma ina vidole vitano vyenye ngozi katikati. Macho yao hayafanyi kazi na yamefunika kwa ngozi. Masikio ni vipenyo vidogo tu.

Spishi [hariri]

Picha [hariri]

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.