Chris Oyakhilome

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chris Oyakhilome (maarufu kama "Mchungaji Chris"; alizaliwa Edo, Nigeria, 7 Desemba 1963) ni "televangelist" na rais mwanzilishi wa Believers' LoveWorld Incorporated ama "Christ Embassy", ambalo ni shirika la Kikristo, makao yake makuu yakiwa jijini Lagos, Nigeria.[1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mchungaji Chris alilelewa katika familia ya Kikristo, aliokoka katika umri wa miaka 9 akaanzisha huduma yake kwa Wakristo kama kijana katika Chuo kikuu cha Bendel State (sasa "Chuo kikuu cha Ambrose Alli") aliposomea ujenzi.[2]

Alimuoa Anita Oyakhilome mwaka wa 1991[3] na wamejaliwa kupata mabinti wawili. Anita alikuwa Mkurugenzi wa ofisi ya kimataifa ya Christ Embassy ambaye pia mchungaji katika makanisa ya Christ Embassy huko Uingereza, ikiwa ni pamoja na sura yake mwenyewe, Embassy Docklands, katika North Woolwich, London. Alikuwa Mkurugenzi-mshiriki wa "Loveworld Christian Network". Mnamo mwaka wa 2016, Mchungaji Chris na Anita walitalikiana baada ya kuishi pamoja kwa miaka 25.[4]

Huduma na uponyaji[hariri | hariri chanzo]

Christ Embassy Luton, Uingereza

Chris Oyakhilome ni mwandishi wa vitabu kadhaa vilivyonunuliwa kwa wingi; kimojawapo kikiwa "Rhapdsody of Realities" ambacho amekiandika pamoja na mkewe, Anita. Mafundisho yake zinapatikana pia katika aina ya sauti na video. Kitabu chake "How to receive your miracle and retain it?" ambacho kinaonyesha maisha ya Mkristo, mamlaka yake kama muumini na mali yote katika ufalme wa Mungu kuwa ni ya kila muumini.

Mbali ya kuongoza mtandao wa makanisa ya Christ Embassy na waumini katika mabara yote matano, Chris huwa pia mchungaji wa shirika kubwa katika Afrika. Yeye husimamia mafundisho na uponyaji mkubwa na makutano ya watu zaidi ya milioni 3.5 katika tukio la usiku mmoja.[5]

Mwaka 2003,alianzisha mtandao wa kwanza wa kikristo barani Afrika kwa dunia mzima na ulijulikana kama LoveWorld Christian Network.[6] Yeye pia ni mwenyeji wa mpango wa programu ya televisheni iitwayo "Atmosphere for Miracles", ambayo ni huwa kuhusu uponyaji ya magonjwa ya kimwili na kiroho na hutangazwa katika mitandao ya matelevisheni kubwa duniani kote.

Mchungaji Chris pia ana Shule ya Uponyaji kama sehemu ya huduma yake.[7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Biography and Achievements of Pastor Chris Oyakhilome -". The NEWS. 2020-05-27. Iliwekwa mnamo 2020-08-22. 
  2. Published. "The Family of Pastor Chris Oyakhilome Revealed". Punch Newspapers (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-08-22. 
  3. Stephanie Obasanho (2020-06-08). "Interesting facts from biography of pastor Anita Ebhodaghe Oyakhilome". Legit.ng - Nigeria news. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-22. 
  4. Obiora Emeka (2013-12-17). "Pastor Chris Oyakhilome, Biography, House, Wife, Children, Private Jet, House, Cars". BuzzNigeria - Famous People, Celebrity Bios, Updates and Trendy News (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-08-22. 
  5. PeoplePill. "Chris Oyakhilome: Global Christian Evangelist | Biography, Facts, Career, Wiki, Life". PeoplePill (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-08-23. 
  6. "About Pastor Chris". BLW Campus Ministry (kwa en-gb). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-06. Iliwekwa mnamo 2020-08-22. 
  7. "A Biography of Pastor Chris Oyakhilome: The Glorious Life of the Man of God". Tribune Online (kwa en-GB). 2019-10-28. Iliwekwa mnamo 2020-08-22. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]