Chikuyu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Chikuyu
Nchi Tanzania
Mkoa Singida
Wilaya Manyoni
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 8,474

Chikuyu ni kata ya Wilaya ya Manyoni katika Mkoa wa Singida, Tanzania yenye msimbo wa posta 43404.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 8,474 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,487 waishio humo.[2]

Imebarikiwa kuwa na idadi kubwa ya wasomi. Wakazi wanajishugulisha na kilimo cha umwagiliaji cha mpunga. Pia watu wake hutumia maji ya mto katika shughuli mbalimbali kama ujenzi n.k. Chikuyu kuna pia umeme na maji ya bomba kutoka mradi wa Konoike.

Kuna shule 3 za msingi pamoja na shule ya sekondari ambayo ilianzishwa mwaka 2000. Pia kuna zahanati moja ambayo hutumika kama kituo cha huduma ya kwanza.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Manyoni - Mkoa wa Singida - Tanzania

Chikola | Chikuyu | Heka | Isseke | Kintinku | Majiri | Makanda | Makuru | Makutupora | Manyoni | Maweni | Mkwese | Muhalala | Nkonko | Sanza | Saranda | Sasajila | Sasilo | Solya


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Singida bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chikuyu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.