Cheti cha Masomo ya Msingi ya Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

KCPE ni ufupisho wa Kenya Certificate of Primary Education, tuzo la cheti kwa wanafunzi baada ya kuhitimu kwa kusoma miaka nane katika elimu ya msingi nchini Kenya. Mitihani yake husimamiwa na [1]Kenya National Examination Council (KNEC), kitengo cha serikali cha kusimamia mitihani nchini Kenya, chini ya Wizara ya Elimu. Kitengo hicho pia husimamia na kufanyia mabadabiriko kwa Cheti cha Masomo ya Upili ya Kenya (KCSE), tuzo la cheti kwa wanafunzi baada ya kumaliza elimu ya sekondari. Vyeti vya KCSE na KCPE vilianzishwa nchini Kenya hapo mwaka wa 1985 wakatmfumo wa elimu wa 8.4.4 ulianzishwa. Maki za juu zaidi ni 500 lakini hiyo aghrabu haiwezekani kutokana na usawasaji (kutolewa kwa baadhi za alama katika kila somo). Mtihani huu hutumiwa kuamua shule ya sekondari ambayo kila mwanafunzi atajiunga nayo.

Jumla ya vipengele vya masomo 5 hutahiniwa. Hizi ni pamoja na: Kiingereza, Kiswahili, Elimu ya Kijamii, Sayansi na Elimu ya Kidini (Ukristo / Uislamu / Uhindi)

Ni muhimu kubainisha kuwa somo la Kijamii hujumuisha vipengele vya masomo katika Historia ya Kenya, elimu ya kisheria na haki na elimu ya Kidini.

Mtihani huu hufanyika wiki pili ya Novemba na inachukua siku nne tu. Kushahihishwa kwa mitihani inayohusisha kuandika (haya ni ya Insha ya Kiswahili na mtungo wa Kiingereza yaani Composition) hufanyika wakati ya likizo ya Desemba. Matokeo kisha hutangazwa na Waziri wa Elimu ya siku 3 au 4 baada ya siku ya Krismasi.