Cherero
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Cherero | ||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Cherero ni ndege wa jenasi Agapornis katika familia Psittacidae. Ndege hawa ni aina ya kasuku wadogo na wana rangi kali. Mkia wao ni mfupi kuliko kasuku wengine lakini kama hawa miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Domo lao lina nguvu sana na mataya yamepindika kwa pande za kuelekea kama koleo. Cherero wanatokea Afrika na Madagaska. Hula matunda, mboga, mbegu na pengine wadudu. Dume na jike wanaishi pamoja kwa maisha yao yote. Hupitisha muda mrefu wakikaa karibu sana. Kwa hivyo huitwa kasuku-mapenzi pia. Jike huyataga mayai 3-8 tunduni kwa mti.
Spishi ya Afrika [hariri]
- Agapornis canus, Cherero Kichwa-kijivu Madagascar au Grey-headed Lovebird)
- Agapornis canus ablectaneus
- Agapornis canus canus
- Agapornis fischeri, Cherero Kichwa-machungwa (Fischer's Lovebird)
- Agapornis lilianae, Cherero wa Lilian (Lilian's au Nyasa Lovebird)
- Agapornis nigrigenis, Cherero Mashavu-meusi (Black-cheeked Lovebird)
- Agapornis personatus, Cherero Shingo-njano (Masked au Yellow-collared Lovebird)
- Agapornis pullarius, Cherero Uso-mwekundu (Red-faced au Red-headed Lovebird)
- Agapornis pullarius pullarius
- Agapornis pullarius ugandae
- Agapornis roseicollis, Cherero Uso-pinki (Peach-faced au Rosy-faced Lovebird)
- Agapornis roseicollis catumbella
- Agapornis roseicollis roseicollis
- Agapornis swindernianus, Cherero Mkufu-mweusi (Black-collared au Swindern's Lovebird)
- Agapornis swindernianus emini
- Agapornis swindernianus swindernianus
- Agapornis swindernianus zenkeri
- Agapornis taranta, Cherero Habeshi (Abyssinian or Black-winged Lovebird)
Picha [hariri]
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cherero kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |