Chechele (Stenostiridae)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Chechele | ||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chechele mkia-mweupe
|
||||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Chechele ni ndege wa familia Monarchidae na Stenostiridae. Zamani wale wa Stenostiridae waliainishwa katika familia Muscicapidae (Culicicapa), Monarchidae (Elminia) na Sylviidae (Stenostira), lakini uchunguzi wa ADN umeonyesha kwamba wana mnasaba na kwa hivyo wamepewa familia yao.
Wana rangi ya buluu (Elminia), ya kijivu (Stenostira) au ya manjano (Culicicapa). Wanatokea misituni au porini kwa vichaka katika Afrika na Asia (Culicicapa). Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika panda ya matawi. Jike huyataga mayai 2.
[hariri] Spishi za Afrika
- Elminia albicauda, Chechele Mkia-mweupe (White-tailed Blue Flycatcher)
- Elminia albiventris, Chechele-kishungi Tumbo-jeupe (White-bellied Crested-flycatcher)
- Elminia albonotata, Chechele-kishungi Mkia-mweupe (White-tailed Crested-flycatcher)
- Elminia longicauda, Chechele Buluu (African Blue Flycatcher)
- Elminia nigromitrata, Chechele-kishungi Mweusi (Dusky Crested-flycatcher)
- Stenostira scita, Chechele Kinyago (Fairy Flycatcher)
[hariri] Spishi za Asia
- Culicicapa ceylonensis (Grey-headed Canary-flycatcher)
- Culicicapa helianthea (Citrine Canary-flycatcher)