Chati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Chati
Chati bega-jeupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Muscicapidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
Jenasi: Cercomela Bonaparte, 1856

Myrmecocichla Cabanis, 1850 Thamnolaea Cabanis, 1850

Spishi: Angalia katiba

Chati ni ndege wa jenasi Cercomela, Myrmecocichla na Thamnolaea katika familia Muscicapidae. Sikuhizi wataalamu wengi wanaainisha spishi za Thamnolaea katika Myrmecocichla. Chati hawana rangi kali isipokuwa spishi za Thamnolaea ambao wana tumbo jekundu. Wengine ni weusi wengine wana rangi ya kijivu au kahawa. Spishi hizi zinatokea Afrika na kadhaa zinatokea Asia ya Magharibi mpaka Uhindi. Kwa kawaida huonekana juu ya miwamba, majabali na vilima vya mawe. Hula wadudu, matunda madogo, mafuta ya wanyama na takataka za kulika za nyumba. Hulijenga tago lao kwa vitu vyororo kama sufu, manyoya na nyuzinyuzi juu ya uoto mfupi au kati ya mawe. Jike huyataga mayai 3-5.

[hariri] Spishi za Afrika

[hariri] Spishi ya Asia

[hariri] Picha

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine