Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi cha Watu wa Ethiopia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi cha Watu wa Ethiopia (Kiamhari: የኢትዮጵያ ሕዝቦች አብዮታዊ ዲሞክራሲያዊ ግንባር Yä-Ityopya Həzbočč Abyotawi Demokrasiyawi Gənbar, kifupi Ih'adeg, Ing: Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front; EPRDF) ni chama cha kisiasa ambacho ni chama tawala cha Ethiopia tangu mapinduzi ya 1991.

Chama hiki ni maungano ya vyama 4 vya kieneo ambayo ni Umoja wa Kidemokrasia wa Watu wa Oromo (Oromo Peoples' Democratic Organization), Harakati ya Kidemokrasia ya Kitaifa ya Amhara (Amhara National Democratic Movement), South Ethiopian Peoples' Democratic Front na Tigrayan Peoples' Liberation Front.

Kiongozi wa chama hiki alikuwa Meles Zenawi aliyeendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa Ethiopia tangu ushindi wa mapinduzi.

EPRDF ilishinda kila uchaguzi tangu 1991. Wapinzani wanadai ya kwamba chama kilitumia mbinu zisizo halali na kubadilisha matokeo ya kweli mara kwa mara pamoja kupeleka wapinzani wengi gerezani.

Tangu uchaguzi wa mwaka 2010 EPRDF imeshika nafasi 499 katika jumla la wabunge 546.