Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Chama cha Kimataifa cha Msalaba Mwekundu)
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ni shirika la kimataifa ambalo ofisi yake kuu iko Geneva, Uswisi. Kamati ilianzishwa na Henri Dunant chini ya jina Kamati ya Watano tarehe 9 Februari 1863. Shabaha zake hasa ni kuwasaidia na kuwalinda watu wakati wa vita. Kamati imezawadiwa Tuzo ya Nobel ya Amani mara tatu: miaka ya 1917, 1944, na 1963.
Siku hizi, kamati ni mwanachama wa Shirika za msalaba mwekundu na hilali nyekundu.
| Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |