Chad (ziwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Chad
Picha za angani zinaonyesha kupungua kwa Ziwa Chad
Picha za angani zinaonyesha kupungua kwa Ziwa Chad
Mahali Afrika ya Kati
Nchi zinazopakana Chad, Kamerun, Nigeria, Niger
Eneo la maji 1500 km²
Kina cha chini hadi 7 m
Mito inayoingia Chari, Komadugu, Logone
Mito inayotoka ---
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
m 240
Miji mikubwa ufukoni --

Ziwa Chad ni ziwa kubwa lisilo na njia ya kutoka lenye kina kidogo katika kanda la Sahel, kando ya jangwa kubwa la Sahara, kule ambako nchi za Chad, Kamerun, Niger na Nigeria zinapopakana, hivi kwamba eneo lake limegawanywa kati ya nchi hizo. Ziwa Chad lina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa watu milioni 68 katika nchi hizo nne.

Beseni lake ni beseni kubwa le bara la Afrika. Hata hivyo, eneo la uso wake limebadilika katika mwendo wa karne zilizopita kutegemeana na kiasi cha maji lilichopokea na kiwango cha uvukizaji na matumizi ya maji yake.

Ziwa Chad lilipungua kwa asilimia 98 baina ya miaka 1963 na 1998 lakini picha za satelaiti za ESA zimeonyesha ya kwamba baada ya hapo limepanuka tena kiasi. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chad (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.