Camping

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Camping msituni pamoja na hema na gari.
Trela ya Camping yenye vitanda, jikoni, bafu na choo ndani yake.
Uwanja wa camping karibu na mji mkubwa wenye wageni wengi wakibanana.
Hao wanabeba vifaa vyote.
Teardrop camper.

Camping (kutoka Kiingereza "camp" = kambi) ni aina ya burudani na pia njia ya utalii ambako watu hutoka katika nyumba zao kwa siku za mapumziko au likizo na kukaa nje.

Mara nyingi watu hutumia hema lakini kuna pia magari maalumu ya camping. Kati ya magari haya kuna matrela yenye vitanda na sehemu ya jikoni na bia magari aina ya basi ndogo ambako sehemu ya abiria imebadilishwa kuwa na vitanda na jiko. Magari ya camping ya hali ya juu huwa pia na choo ndani yao.

Kama hali ya hewa ni nzuri bila hofu ya mvua watu kadhaa hupenda kulala nje moja kwa moja hata bila hema.

Camping kama burudani ilianza kuenea katika nchi zilizoendelea tangu mwanzo wa karne ya 20. Kulala katika hema kama njia ya maisha jinsi ilivyo kati ya vikundi vingi vya wahamiaji na wafujai haiitwi camping.

Katika nchi nyingi kuna mahali pa pekee panapoandaliwa kama uwanja wa camping. Mara nyingi huwa na nafasi za kuoga, kupika na choo, pamoja na duka. Nafasi zimeandaliwa kwa kila hema. Kama pameandaliwa kupokea pia magari ya campig huwa pia na umeme kile sehemu. Kukaa kwenye uwanja wa camping ni bei nafuu kuliko kulala katika hoteli au nyumba ya wageni kwa hiyo ni hasa vijana au watu wasio na pesa nyingi sana wanaotembelea hapa. Wengine hupendelea kutumia pesa yao kwa kununua gari la camping na kuwa na uhuru zaidi wa kutembea wakati wa likizo jinsi wanavyopenda.

Nchi penye maeneo makubwa bila wakazi wengi huwa pia na makambi ya camping katika hifadhi zua kitaifa ambako nafasi mara nyingi ni za duni zaidi.

Kuna pia ambako vibanda vidogo vianatikana kwa wageni kwenye uwanja wa camping.

Vifaa vya camping[hariri | hariri chanzo]

Desturi ya camping imezaa biashara ya vifaa vilivyobuniwa hasa kwa manufaa ya watu wanaofanya camping. Vifaa hivi hupangwa kuwe nyepesi, vinatakiwa kuchukua nafasi ndogo, na vingine vinawez kukujwa.

Vifaa hivi ni, kwa mfano, pamoja na:

  • Hema au teardrop camper ya kubebea vitu na kulala
  • Mfuko wa kulala
  • Mgodoro wa hewa au mkeka wa plastiki
  • Jiko la kubebwa
  • Sufuria zinazoingiliana
  • Kifurushi cha Msaada wa Kwanza
  • Choo cha kikemia (kwenye gari la camping)
  • Tochi
  • Viti vya kukunja
  • Akiba ya kamba
  • Viatu maalumu kwa matembezi ya mbali
  • Dawa ya mbu
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Camping kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.