Cadimi
| Cadimi au Kadimi (Cadmium) |
|
|---|---|
|
|
|
| Jina la Elementi | Cadimi au Kadimi (Cadmium) |
| Alama | Cd |
| Namba atomia | 48 |
| Mfululizo safu | Metali ya mpito |
| Uzani atomia | 102.9055 |
| Valensi | 2, 8, 18, 18, 2 |
| Densiti | 112.411 g/cm³ |
| Kiwango cha kuyeyuka | 594.22 K (321.07 °C) |
| Kiwango cha kuchemka | 1040 K (767 °C) |
| Asilimia za ganda la dunia | 10-5 |
| Hali maada | mango |
| Mengineyo | metali haba |
Cadimi (pia: Kadimi - kupitia Kilatini "Cadmium" kutoka Kigiriki καδμεία kadmeia iliyotaja mitapo yenye cadimi kwa heshima ya mungu wa Kigiriki Κάδμος Kadmos) ni elementi na metali haba duniani. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Cd na namba atomia 48 katika mfumo radidia.
Tabia na matumizi [hariri]
Cadimi ni metali laini yenye rangi nyeupe-buluu. Hufanana mara nyingi na tabia za zinki lakini humenyuka kirahisi zaidi. Cadimi yenyewe na kampaundi zake huwa ni sumu ikisababisha kansa.
Matumizi yake ni hasa katika beteri, viungo vya rangi na teknolojia ya kinyuklia.
Nondo za Cadimi zilitumiwa 1942 na Enrico Fermi katika tanuri nyuklia ya kwanza kwa kusidi la kutawala mmenyuko mfulizo wa nyuklia. Nondo hizi zilisukumwa kati ya nondo za urani na kupunguza mwendo wa nyutroni kati ya nondo za urani.
| Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cadimi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |